Skip to main content

Posts

Recent posts

Lukuvi afunga ofisi nzima, ageukia wamiliki viwanja

 Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, William Lukuvi jana alifunga ofisi za ardhi na masijala za Jiji la Dar es Salaam, akisema anafunga mtambo wa kufyatua migogoro ya ardhi. Waziri Lukuvi pia amewaonya wamiliki katika Mradi wa Viwanja 20,000 kukaa chonjo kwa kuwa wanaweza kunyang’anywa, huku akiagiza kuanza kwa msako wa watu waliotelekeza hati 6,000 za umiliki wa viwanja zilizotolewa na wizara yake takribani miaka 20 iliyopita. Lakini, moto ulikuwa ofisi ya ardhi ya Jiji la Dar es Salaam ambako Waziri Lukuvi alitaka maofisa hao wakusanye nyaraka za ofisi yao na kuhamia wizarani kwa kuwa hawana cha kufanya eneo hilo. “Mnajua kwa muda mrefu nimekuwa nikipambana na migogoro ya ardhi nchini, leo imefika tamati. Nimeshagundua chanzo chake kinatokea hapa. Nazifunga hizi ofisi,” alisema Waziri Lukuvi. “Hizi ofisi zinatoa hati zisizotambulika kwa kisingizio cha ofa. Mtu yeyote mwenye ofa ya kiwanja na ina muhuri wa jiji haitambulik...

CAR FROM JAPAN

http://click.carfromjapan.com/track/click/30577300/carfromjapan.com?p=eyJzIjoiTFQ2OF9jcldlNVZ4MGNmLWtnUHFYX2hwck8wIiwidiI6MSwicCI6IntcInVcIjozMDU3NzMwMCxcInZcIjoxLFwidXJsXCI6XCJodHRwczpcXFwvXFxcL2NhcmZyb21qYXBhbi5jb21cXFwvZW5cXFwvY2FtcGFpZ25cXFwvZ2l2ZWF3YXkteG1hcy0yMDE2P3JlZmVyPTU4NDFkMmMzMWExZjg5MDEwMDc4NDA3ZCZ1dG1fbWVkaXVtPWVtYWlsJnV0bV9zb3VyY2U9dHJhbnNhY3Rpb25hbCZ1dG1fY2FtcGFpZ249Y2FtcGFpZ24td2VsY29tZVwiLFwiaWRcIjpcIjAyMGE0ZjgwMTkxMjQ4N2I4NDc3NDUwNGYyOGRlMjA3XCIsXCJ1cmxfaWRzXCI6W1wiYmQ3ZGM4ZDg0ODc1NWU5MzAyMDY3Njc3ZjY2Njc5ZWQ2NjE2MzIwNVwiXX0ifQ

Membe kupeleka nchi kwenye uchumi wa viwanda

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ametangaza rasmi kuwania urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM}, huku akitamba ataipeleka nchi katika uchumi wa viwanda unaobebwa na kilimo na kuahidi kujenga serikali ya waadilifu. Licha ya Membe, wana CCM wengine wawili jana walitangaza pia kugombea urais nao ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Januari Makamba pamoja na Mbunge wa Nzega Dk Hamis Kigwangala. Membe alifichua kuwa alienda kuomba kwenye kaburi la Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere ili kupata ridhaa na kusisitiza kuwa urais si suala la kukurupuka na kwamba atahakikisha anasimamia utawala bora, huku akiongoza mapambano dhidi ya rushwa na kwa kubadili kipengele cha mtu atakayetoa rushwa na kutoa taarifa awe huru. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya CCM Mkoa wa Lindi jana, Waziri Membe alisema kabla ya kuchukua uamuzi wa kufikiria urais alijipima na kuona anatosha kwa nafasi hiyo, pia baada ya kuwaangali...

Mama amchoma mikono mwanae kwa madai ya kuiba ugali

i Mponzi mkazi wa kijiji cha Ikule wilayani Kilombero,  mkoani Morogoro anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma mwanae na kumjeruhi mikono kwa madai ya kuiba ugali. Mama huyo alimuunguza mwanaye  Joseph Chawala, akimtuhumu Kuiba Ugali, kwa mujibu wa watendaji  mbalimbali wa kata ya Mng’eta. Wakizungumzia tukio hilo Jerome Chulu na Jeneth Hetela,  walisema unyanyasaji huo  ulishuhudiwa na majirani wa mwanamke huyo baada ya kusikia kelele za watoto ambao walimchukua mtoto huyo kumpeleka ofisi  ya mtendaji wa kata,polisi na baadaye hospitali. Walibainisha baadaye kuwa polisi  walikwenda kumkamata mwanamke huyo na mumewe Halidi Kiwenji ambaye  inadaiwa alikuwa karibu wakati wa tukio hilo ingawa baadaye baba huyo aliachiwa ili akawaangalie watoto wengine nyumbani. Polisi  walithibitisha tukio hilo ambalo uchuguzi wake unaendelea ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo. Wananchi mbalimbali waliohojiwa wametaka hatua kuchukuliw...