Skip to main content

Sumatra kiini cha ajali barabarani

WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema ajali za barabarani zinachangiwa na uzembe wa taasisi inayosimamia sekta ya usafiri jambo linalogharimu maisha ya watu wasio na hatia, na kuitaka taasisi hiyo kuchukua hatua na kuhakikisha nidhamu inarejea kwenye sekta hiyo.

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) ndiyo yenye dhamana ya kusimamia na udhibiti wa sekta ya usafiri katika nchi kavu na majini.

Sitta aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari wakati Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipokuwa ikizungumza na viongozi wa wizara hiyo.

Sitta alisema “Hakuna kitu kinachoniuma kama ajali za barabarani ambazo nyingi zinasababishwa na uzembe, ubovu wa magari na matairi ya mtumba, halafu baya zaidi ni kwamba Mamlaka husika ya kudhibiti vyombo hivyo ipo, inaona na kuwasamehe makosa,” alisema Sitta.

Aliongeza, mamlaka husika zina wajibu wa kusimamia vyombo hivyo na kuhakikisha vile vinavyofanya makosa vinachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuvifutia leseni, kwani matukio mengi ya ajali yanatokana na uzembe na kuanzia sasa masuala ya msamaha yasiwepo.

“Hatuwezi kuendelea kuona wananchi wanakufa tu, kwa sababu ya uzembe wa madereva au wamiliki, nilizungumza na baadhi ya wamiliki wanasema hawawezi kununua matairi mapya, kwa sababu ya gharama, wanatumia matairi ya mtumba, sasa jambo hili sio sahihi, kama hawawezi kutoa huduma kwa kutumia vyombo vyenye viwango, waache, na sio kucheza na uhai wa watu,” alisisitiza Sitta.

Sitta aliongeza, wamiliki wa vyombo vya moto na madereva, wanapaswa kufuata sheria za barabarani na kuhakikisha wanazitii na kwamba vyombo hivyo vinapaswa kuwa na vipuri vyenye viwango na kuhakikisha mabasi yanayokwenda umbali zaidi ya kilometa 700, yawe na madereva wawili.

“Ipo sheria inayozungumzia umbali unaotakiwa dereva mmoja aendeshe gari, lakini pia nilizungumza na daktari kuhusu umbali unaokubalika kwa madereva kuendesha chombo cha moto, aliniambia dereva mmoja hatakiwi kuendesha gari kwa umbali wa zaidi ya kilometa 700, zaidi ya hapo inabidi wawe madereva wawili,” alisema Sitta.

Alisema hiyo inatokana na ukweli kwamba kwa umbali huo, wa kilometa 700 dereva huwa amechoka na akienda zaidi ya hapo anaweza kusababisha ajali kwa kuwa akili na mwili vimechoka hivyo hawezi kuwa makini barabarani.

Akizungumzia ubovu wa mabasi ya abiria na daladala, Sitta alisema magari yote mabovu, yanapaswa yasiwepo barabarani, kwani kuwepo kunachangia ajali kwa njia moja au nyingine.

Kuhusu mgomo, Sitta alisema nchi inaongozwa kwa sheria na kwamba sio kila kitu kinachofanywa na serikali ni masuala ya siasa, hivyo sio sahihi madereva na wamiliki wa mabasi kugoma kutoa huduma kwa abiria.

‘Huwezi kugoma kutoa huduma kwa abiria, halafu madereva wanatoa amri kwa serikali eti wanatoa siku kadhaa madai yao yatekelezwe, hii ni nchi inayoongozwa kwa sheria na sio vitisho, hawana haki ya kufanya hivyo, wanachotakiwa ni kufuata sheria,” alisema Sitta.

Alisema kama kuna madai ya stahiki za madereva na wamiliki wa vyombo hivyo, wanapaswa kupeleka madai yao sehemu husika na kwamba tatizo kubwa linaloonekana kwa watu hao ni usaliti wa wao kwa wao.

Alisema mfumo wa malalamiko upo na kwamba kama waliona uamuzi wa kushusha nauli sio sahihi, walipaswa kukata rufaa, jambo ambalo wamelifanya na kusubiri rufani yao ndani ya siku 14.

“Hii nchi inaongozwa na sheria, kama wamiliki waliona uamuzi wa kushusha nauli sio sahihi walipaswa kukata rufaa, jambo ambalo wamefanya na wasubiri uamuzi wa rufani yao ndani ya muda huo, na majibu ya rufani yanaweza kukubaliwa au kukataliwa,” alisema Sitta.

Aprili 15 mwaka huu serikali ilitangaza viwango vipya vya nauli ambavyo vilitarajiwa kuanza kutumika jana Aprili 30, mwaka huu kwa kushusha nauli za mabasi ya mikoani huku nauli za daladala zikibaki palepale

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...