Written by Grace Mkojera
Hits: 26
UONGOZI wa Azam FC umesema hautarajii kuajiri mtu mwingine kwa ajili ya kusimamia cheo cha Meneja na badala yake nafasi hiyo atakabidhiwa Kocha mpya ajaye.
Nafasi hiyo ya Meneja awali ilikuwa ikishikiliwa na Jemedari Said ambaye amemaliza mkataba wake na klabu hiyo na kupata ajira mpya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kama Ofisa maendeleo wa soka la vijana.
Akizungumza jana Dar es Salaam Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC Saad Kawemba alisema Kocha mpya ajaye ndiye atakuwa Meneja na kwamba atakuwa akisimamia masuala yote ya timu.
“Hatutegemei kuajiri Meneja mwingine zaidi tunategemea kuwa Kocha mpya tunayemtafuta ndiye atakuwa Meneja wa timu, tumeondokana na mfumo huo wa zamani tuendane na mfumo mpya,” alisema.
Katika nchi zilizoendelea nafasi ya Meneja huwa ni ya Kocha mwenyewe, mfumo ambao Azam wameamua kuja nao.
Kocha anayetarajiwa kupewa nafasi hiyo ni Stewart Hall ambaye aliwahi kuitumikia timu hiyo msimu wa mwaka 2012/2013 na 2013/2014 hadi aliponyang’anywa mikoba na Mcameroon Joseph Omog.
Kocha mwingine ambaye anatajwa kupewa nafasi Azam FC ni Goran Kopunovic ambaye ilidaiwa bado hajaafikiana na uongozi wa Simba ili kusaini mkataba mpya.
Kopunovic ameiongoza Simba nusu msimu baada ya kuchukua mikoba ya Mzambia Patrick Phiri. Kocha huyo ndiye aliyekisaidia kikosi hicho kumaliza msimu katika nafasi ya ta
Comments
Post a Comment