Skip to main content

Azam yamrejesha Hall

UONGOZI wa klabu ya Azam umeamua kumrejesha kocha Sterwart Hall kwa ajili ya kuiongoza timu hiyo kwenye msimu ujao wa ligi na michuano ya kimataifa.

Habari za uhakika zilizopatikana kutoka ndani ya uongozi wa Azam Dar es Salaam jana, zilisema uongozi umeona Hall bado ana nafasi kwenye klabu hiyo.

“Ni kweli Hall anarudi Azam na jana (juzi) tumemalizana naye, anatarajia kuanza kazi rasmi Juni 15 siku ambayo timu itarudi kambini… maana kwanza ametuomba akatoe notisi kwenye ofisi yake Sunderland."

Hall ni mwajiriwa katika Kituo cha Michezo cha Kidongo Chekundu kinachojengwa kwa ushirikiano na kampuni ya umeme ya Symbion na klabu ya Sunderland ya Uingereza kwa ajili ya kuinua kipaji.

Mtoa habari wetu aliliambia gazeti hili kuwa kocha Hall anarudi kwenye nafasi yake ya ukocha mkuu huku George Nsimbe na Dennis Kitambi wakiwa wasaidizi wake.

“Mambo yote yameshakamilika Hall anasubiriwa kuanza kazi tu na wasaidizi wake watakuwa Nsimbe na Kitambi, hatutawabadilisha hao,” alisema. Hall anarudi Azam kwa mara ya tatu sasa.

Aliitumikia katika vipindi viwili tofauti, ambapo mara ya kwanza ikiwa ni katika msimu wa mwaka 2012/2013 alipoiongoza kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Bara na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Sababu za kuondoka msimu huo ilikuwa ni kutoelewana na uongozi baada ya kocha huyo kumpanga Mrisho Ngassa (aliyekuwa Azam wakati huo) katika mechi ya fainali ya Kombe la Kagame Julai 2012, ambapo Azam ilicheza na Yanga na kufungwa kwa mabao 2-0.

Hall alirudi tena Azam katika msimu wa mwaka 2013/2014 na kuiongoza timu hiyo katika mechi zote za raundi ya kwanza kabla ya uongozi wake kutangaza kusitisha mkataba naye kwenye mechi ya mwisho ya raundi ya kwanza iliyochezwa Chamazi na kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mbeya City.

Mcameroon Joseph Omog ndiye aliyechukua mikoba ya Hall na kuiongoza Azam katika mzunguko wa pili msimu huo, ambao timu hiyo ilicheza bila kupoteza mechi na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza.

Omog na msaidizi wake, Ibrahim Shikanda waliiongoza Azam katika msimu wa ligi wa mwaka 2014/2015 kabla ya kufutwa kazi Februari mwaka huu baada ya Azam kutupwa nje ya michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika na timu ikawa chini ya Nsimbe na Kitambi, ambao waliiongoza kumaliza nafasi ya pili katika ligi.

Katika hatua nyingine, Azam imemuongezea mkataba wa miaka miwili mchezaji wake Salum Abubakar huku ikimalizana na Erasto Nyoni na Said Morad ambao wanatarajiwa kusaini mkataba muda wowote.

Aidha, timu hiyo imesitisha mkataba wake na David Mwantika na imeshamlipa stahiki zake zote na kwamba yupo huru baada ya kutoridhika na kiwango chake.

“Azam ilisaini mkataba wa miaka miwili na Mwantika na unatarajia kumalizika Novemba, baada ya majadiliano ikaonekana bora kusitisha mkataba na mchezaji huyo ili awe huru na kutafuta timu nyingine,” alisema kiongozi huyo. Mwantika alijiunga na Azam FC akitokea Prisons ya Mbeya

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...