Skip to main content

CAG aikalia kooni Serikali

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, ameamua kuiorodheshea Serikali mapendekezo yote ya mtangulizi wake, Ludovic Utouh, ambayo hayajatekelezwa na Serikali tangu 2008 na kusisitiza sasa yatekelezwe.

Katika mapendekezo ya mwaka 2009/2010, Profesa Assad, amelalamikia kitendo cha Serikali kuendelea kuruhusu mwanya wa mgongano wa maslahi, kwa kuendelea kuteua wabunge kuwa wajumbe wa bodi za mashirika na taasisi za umma.

“Bunge ndio chombo cha juu kinachowakilisha wananchi na chenye majukumu ya kutathimini utendaji kazi wa Serikali, ikiwa ni pamoja na mashirika na taasisi nyinginezo za umma kupitia kamati za kudumu za Bunge.

“Ili kuepuka mgongano wa kimaslahi, nasisitiza mapendekezo yangu kuwa, wabunge hawastahili kuteuliwa kuwa wajumbe wa bodi za wakurugenzi katika mashirika na taasisi nyinginezo za umma, kwani wana jukumu la kusimamia mashirika hayo,” amesema Profesa Assad.

Posho sawa Akielezea mapendekezo ya mwaka 2008/2009 ambayo hayajafanyiwa kazi, Profesa Assad ameitaka Serikali kuhakikisha kuwa kuna uwiano katika marupurupu wanayopata menejimenti na bodi za wakurugenzi za taasisi za umma.

“Hii inatokana na ukweli kuwa rasilimali wanazotumia kama posho za vikao, ada za bodi za wakurugenzi na nyinginezo, ni rasilimali za umma,” alisema Profesa Assad.

Alisema hatua ya Serikali kuanzisha Bodi ya Uwiano wa Mishahara na Marupurupu, itasaidia kuondoa tofauti zilizopo sasa za kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika mashirika na taasisi nyinginezo za umma.

Wanaodaiwa Bodi ya Mikopo Kuhusu kutorejeshwa kwa mikopo ya Sh bilioni 51, iliyokopwa na wanafunzi wa zamani wa vyuo vikuu, ambao sasa hivi ni waajiriwa au wamejiajiri, Profesa Assad aliishauri Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuwachukulia hatua za kisheria waajiri na wakopaji binafsi, ambao hawatoi ushirikiano.

Alitaka hatua hiyo ichukuliwe kwa kuzingatia Sheria Namba 9 ya Bodi hiyo ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Kuhusu mkopo uliokopeshwa katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu wa Sh bilioni 54 kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Wanafunzi wa Umma (PSPF), alitaka Serikali irejeshe mkopo wote na riba.

Adhabu TPA Kuhusu mapendekezo ya mwaka 2010/2011, Profesa Assad alirejea ukaguzi wa mwaka huo, uliobaini kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ilifanya ununuzi wa dharura milioni 13 bila idhini kutoka kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali. “Sina taarifa ya hatua zilizochukuliwa kuhusu suala hilo la ununuzi wa dharura wa Mamlaka ya Bandari Tanzania,” amesema.

Katika mwaka huo huo, Profesa Assad alihoji kwa nini Waziri wa zamani wa Kilimo, Hifadhi ya Chakula na Ushirika, ameendelea kukaa katika nyumba ya Bodi ya Sukari Tanzania, iliyopo Kiwanja 482 Barabara ya Bray Masaki.

Mgogoro wa UDA Profesa Assad pia aliendelea kuhoji uuzwaji wa hisa za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), uliofanywa na Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo bila kupata kibali cha Serikali. Alisema hisa za UDA zilikuwa na thamani ya Sh 744.79 kila hisa Oktoba 2009 na ilipofika Novemba 2010 thamani ya kila hisa ikawa Sh 656.15.

Kwa mujibu wa Profesa Assad, katika uuzwaji wa hisa hizo, Bodi ya Wakurugenzi iliamua kutoa punguzo la asilimia 60 kwa kila hisa, bila kuwepo kwa sababu ya kufanya hivyo.

Profesa Assad alieleza kuwa Mlipaji Mkuu wa Serikali alipoulizwa, alisisitiza kuwa hatambui uuzwaji wa hisa hizo na Serikali inaandaa mapendekezo ya kuuza asilimia 49 ya hisa za UDA, na itafikisha mapendekezo hayo katika Baraza la Mawaziri.

“Majibu haya (ya Mlipaji Mkuu wa Serikali), hayasemi chochote kuhusu mustakabali wa hisa ambazo zilishauzwa na hatua zilizochukuliwa dhidi ya wakurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa UDA,” alisema.

Benki ya Azania Profesa Assad pia alihoji inakuwaje mashirika ya pensheni yameanzisha Benki ya Azania, halafu benki hiyo ikaanzishwa kama kampuni binafsi na kuachwa kuwa katika orodha ya mashirika yanayosimamiwa na Msajili wa Hazina.

Kwa mujibu wa Profesa Assad, benki hiyo ambayo awali iliitwa 1st Adili Bancorp Limited, wanahisa wake ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hisa asilimia 34.8, Mfuko wa Pensheni wa PPF hisa asilimia 30.1, Mfuko wa Pensheni wa PSPF hisa asilimia 17.2, Mfuko wa Pensheni wa LAPF hisa 14.2, Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) hisa 2.3 na wafanyakazi wa Benki ya Azania na wanahisa wengine wenye asilimia 1.4.

CAG katika hilo aliweka wazi kuwa mifuko ya pensheni, ndiyo yenye hisa nyingi sawa na asilimia 96.3, na hivyo ndiyo yenye nguvu ya kutoa miongozo na kusimamia benki hiyo na kwa kuwa mifuko yote ya pensheni inamilikiwa na Serikali, ni wazi benki hiyo ni mali ya Serikali.

Kutokana na mazingira hayo, Profesa Assad alihoji kwa nini benki hiyo haijawahi kuwasilisha hesabu Zake katika ofisi ya CAG tangu 1995 ilipoanzishwa, kwa ajili ya ukaguzi kama Katiba inavyotaka.

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...