NYOTA wa muziki wa bongo flava nchini, Diamond Platinumz amewataka wasanii wa Tanzania kusambaza nyimbo zao kwa njia ya teknolojia ili kunufaika na jasho lao.
Diamond aliyasema hayo wakati akizindua teknolojia ya muziki ili kuziingiza sokoni kazi zake baada ya kushauriana na wadau anaoshirikiana nao kikazi ambayo pia yeye ni balozi anayeitangaza.
Amesema sababu kubwa iliyomsukuma kufanya biashara ya muziki kupitia progamu hii ni kwamba nyimbo zake ziweze kuwafikia mashabiki wake popote na muda wowote kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi na anakuwa na uhakika wa kupata mapato tofauti na zinavyosambazwa na wasambazaji wa mtaani.
“Duniani kuna ushindani katika nyanja zote, hivyo sisi wanamuziki wa Tanzania tunapaswa kuhakikisha tunatoa muziki wa viwango vya juu kuhakikisha tunalenga zaidi katika masoko ya ndani na nje kama wenzetu wanavyofanya kusambaza kazi zao kupitia kampuni zinazotumia teknolojia ya kisasa na kumnufaisha msanii.
“Kuna umuhimu mkubwa wa kujiamini, kufanya vizuri ili tuweze kutangaza Tanzania, kutangaza lugha ya Kiswahili na kupata mapato ya kutosha kutokana na kazi ya muziki, ambayo ikifanywa kitaalamu inalipa kwa kiasi kikubwa,” alisema Diamond
Comments
Post a Comment