Skip to main content

‘Friends of Lowassa’ kuchangia damu Muhimbili

MAKAMU Mwenyekiti wa marafiki wa Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Angel George, amesema mipango imekamilika ya kwenda kuchangia damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

George alitoa taarifa hiyo jana jijini hapa, baada ya kusoma taarifa kwenye vyombo vya habari ikieleza kwamba, Hospitali ya Taifa Muhimbili inakabiliwa na uhaba wa damu.

“Hii taarifa tumeiona, tayari tumewasiliana na marafiki wa Lowassa waitwao Friends of Lowassa nchi nzima na naamini tukimaliza kikao leo, safari ya kwenda kuchangia damu kule Muhimbili ili kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu itakuwa tayari.

“Kwa hiyo naomba nitumie fursa hii kuwaomba Watanzania wenzetu wanaojali na kuthamini maisha ya Watanzania wote, wajitokeze ili kufanikisha uchangiaji wa damu,” alisema George.

“Sisi ambao ni marafiki wa Lowassa, tumeamua kufanya shughuli hizo za kuisaidia jamii ili kumuunga mkono na kumhamasisha Lowassa anayetarajiwa kutangaza nia hivi karibuni ya kuwania urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

“Hii ndiyo hamasa yetu kwake sisi marafiki zake na tumeamua kuisaidia jamii kwa kuchangia damu ili kuitanguliza jamii mbele. Lakini hata kwake ni hamasa kwamba akifanikiwa kuingia Ikulu, jamii iwe ya kwanza,” alisema.

Kupitia vyombo vya habari juzi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha, alisema hospitali hiyo imekumbwa na uhaba wa damu hatua ambayo imelazimu kuomba msaada wa dharura serikalini na kwa watu binafsi.

Alisema uongozi wa hospitali hiyo umewaomba Watanzania, mashirika ya umma, kampuni na watu binafsi, kujitokeza kwa wingi ili kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa wanaopelekwa hospitalini hapo.

“Kwa siku Hospitali ya Taifa ya Muhimbili huhitaji wastani wa chupa za damu 70 hadi 100 na hii inachangiwa na ongezeko la mahitaji ya damu ambayo hutumika zaidi kwa wagonjwa wa dharura, wajawazito, wagonjwa waliofanyiwa upasuaji, watoto na wagonjwa wa saratani,” alisema Aligaesha.

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...