Skip to main content

Kapuya apinga Kiswahili kutumika kufundishia

SERIKALI imehadharishwa kutowatenga Watanzania na ulimwengu kwa kutekeleza sehemu ya Sera ya Elimu, inayotaka Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia kutoka shule ya awali mpaka chuo kikuu.

Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya, ametoa hadhari hiyo bungeni jana wakati alipokuwa akichangia katika mjadala wa makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu unaoendelea.

Profesa Kapuya alikumbusha maoni ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliposema kuwa Ki ingereza ndio Kiswahili cha dunia. Profesa Kapuya amewahi kuwa waziri wa elimu na mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alionya kuwa Watanzania watafanya kosa kubwa litakalowagharimu katika Jumuiya za kikanda hasa katika ushindani wa ajira, kama wataondoa Kiingereza kuwa lugha ya kufundishia.

Alitoa mfano wa nchi ya Rwanda, ambayo imebadilisha lugha ya kufundishia kutoka Kifaransa kwenda Kiingereza na kuongeza; “Nenda pale Rwanda uone mtoto wa darasa la saba anavyozungumza Kiingereza kizuri.”

Aliwajia juu wanaoshabikia Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia kutoka shule ya awali mpaka chuo kikuu, kwamba ni wanafiki kwa kuwa wenyewe watoto wao wamewapeleka katika shule za mchepuo wa Kiingereza.

Alisema watua hao wamekuwa wakitoa mfano wa China na Japan, lakini wanasahau kuwa nchi hizo zina historia tofauti ya elimu ikilinganishwa na nchi za Afrika hususani Tanzania.

“Kule Afrika Kusini wakati wa mauaji ya Soweto, moja ya madai ya Waafrika Kusini ni kuacha kufundishwa kwa kutumia lugha ya Afrikaans na Kizulu, na badala yake wafundishwe kwa Kiingereza ili wawe sehemu ya ulimwengu,” alisema Profesa Kapuya.

Alionya kuwa kama Serikali itaendelea na mpango huo wa kutekeleza sehemu ya Sera ya Elimu ili Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia, hatari ya kwanza itakuwa kulazimisha baadhi ya watu kujifungia na kuanza kutafsiri mawazo ya watu.

Alifafanua kuwa kwa mazingira hayo, itakuwa sawa na kulazimisha watu kutunga vitabu, wakati kiuhalisia watu hujiamulia kuandika vitabu wenyewe.

Hatari ya pili kwa mujibu wa Profesa Kapuya, ni kuwanyima Watanzania hasa waliomaliza vyuo vikuu, wigo wa kujisomea vitabu mbalimbali na kupata maono na kujiwekea dira zao binafsi.

Profesa Kapuya aliwahi kuwa Waziri wa Elimu, Utamaduni na Michezo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana.

Alihitimu Shahada yake ya Sayansi katika Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1971 na pia Shahada ya Pili ya Sayansi katika Botani katika chuo kikuu hicho mwaka 1972.

Alipata Shahada ya Udaktari wa Falsafa katika Botani katika Chuo Kikuu cha Wales Aberystwyth.

Baada ya kuhitimu UDSM, Profesa Kapuya aliajiriwa moja kwa moja kufundisha katika chuo kikuu hicho, akianzia Mhadhiri Msaidizi wa Botani, Mhadhiri, Mhadhiri Mwandamizi hadi Profesa wa Botani.

Aligombea ubunge wa Urambo Magharibi mwaka 1995 na kushinda. Alishinda tena ubunge katika uchaguzi wa 2000, 2005 na 2010.

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...