Skip to main content

Katiba mpya ilivyoleta mgawanyiko ndani ya jamii

Wahenga walisema dalili ya mvua ni mawingi. Usemi huo umejidhihirisha kwenye mchakato wa mabadiliko ya Katiba ambao tayari umeonyesha kuligawa taifa katika makundi matatu; Serikali, taasisi za dini na vyama vya siasa.

Dalili za vikwazo vya kukamilika kwa mchakato huo zilianza kuonekana wakati wa Bunge la Katiba, ambako April 16 mwaka jana, wabunge zaidi ya 200 wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), walisusia vikao vya Bunge hilo na kutoka nje.

Hata hivyo, hatua hiyo haikuonekana kuathiri Bunge hilo kwa kuwa wajumbe wengine kutoka taasisi mbalimbali, kikiwamo chama tawala CCM, United Democratic (UDP), Tanzania Labour (TLP) na UPDP, waliendelea na mjadala.

Bunge hilo lilimalizika baada ya kupata zaidi ya theluthi mbili ya kura kutoka pande zote mbili za Muungano, yaani Tanzania Bara na Zanzibar, licha ya wajumbe wa Ukawa kulisusa.

Kitendo cha Ukawa kususia Bunge la Katiba kilionekana kuchochea taasisi zingine kutoa matamshi mbalimbali ya kutishia kuususia mchakato huo kama ifuatavyo;

Jumuia na Taasisi za Kiislamu

Mapema Februati mwaka huu, Jumuia na Taasisi za Kiislamu zipatazo 11, zikiwamo Baraza Kuu, Tampro, Basuta, Jasuta, IPC, Haiyat Ulamaa na Shura ya Maimamu Tanzania, zilitangaza kuwa zitafanya kampeni za kuhamasisha wanajumuia wake kususia kupiga Kura za Maoni ya Katiba Inayopendekezwa hadi pale watakapopata uhakika wa uwepo wa Mahakama ya Kadhi yenye meno.

Tangazo hilo lilitolewa na Naibu Katibu wa Jumuia ya Shura ya Maimamu Wilaya ya Kinondoni, Rajab Katimba.

Jumuia hizo zikaeleza kuwa kinachoendelea katika mchakato wa upatikanaji wa Mahakama ya Kadhi, ni mwendelezo wa ulaghai ambao umekuwa ukifanyika miaka yote hasa kinapofika kipindi cha kupiga kura kwa lengo la kupata kura za waumini hao.

Shehe Katimba anasema kuna baadhi ya taasisi za kidini na vyombo vya habari vinapotosha kuwa Mahakama ya Kadhi italeta vurugu.

Anasema kwamba Mahakama hiyo inatuhumiwa kuwa itatoa adhabu za kikatili, ikiwamo kukata watu mikono, kuhukumu wasiokuwa Waislamu na kuwabagua wasiokuwa Waislamu.

Shehe Abdallah Bawazir ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Hay Atul-Ulamaa, akasema katika taarifa rasmi ya Jumuiya hiyo kuwa muswada unaojadiliwa ili kupatikana Mahakama ya Kadhi ni kiini macho.

Bawazir katika taarifa hiyo anafafanua kuwa muswada huo unaitaka Mahakama ya Kadhi ijiendeshe yenyewe bila kupata fedha kutoka Serikalini kitu ambacho hakiwezekani.

“Zipo mahakama za makundi ya watu maalumu ambazo zinaendeshwa kwa pesa za Serikali ambazo ni kodi za Watanzania wote. Mfano ni kama vile Mahakama ya Kazi, Ardhi na Mahakama ya Biashara. Kwa nini mahakama itakayotafsiri sheria za Kiislamu iwe nongwa?” alihoji.

Tamko la viongozi wa PCT

Machi 12, mwaka huu, Jukwaa la Kikristo Tanzania (PCT) linaloundwa na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) lilitoa tamko la kutounga mkono Katiba Inayopendekezwa likidai kuwa katiba hiyo imeandaliwa katika mazingira yasiyokuwa ya kiuadilifu.

Waraka wa baraza hilo, kwa vyombo vya habari ulisainiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa kwa niaba ya (CCT), Rais wa Baraza la Maaskofu Katholiki Tanzania Tracius Ngalalekumtwa (TEC) na Daniel Aweti kwa niaba ya Wapentekoste (CPCT).

Katika tamko hilo PCT ilibainisha kwamba kutokana na hali hiyo, kanisa haliwezi kuunga mkono kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa, hivyo liwataka waumini wao kuipigia kura ya hapana.

Jukwaa hilo limeeleza kuwa Katiba Inayopendekezwa haijajibu matakwa na malalamiko ya wananchi kwenye masuala mbalimbali yanayohusu muundo wa Serikali, miiko na maadili ya viongozi wa umma, uwiano wa mihimili ya dola, madaraka ya Rais na haki za binadamu.

“Kanisa haliwezi kuunga mkono kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa kutokana na hali hii, hivyo basi Jukwaa linawataka waumini wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya hapana,” ikasema sehemu ya taarifa hiyo.

Hatua ya Serikali

Siku chache baada ya kauli ya viongozi hao, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe alitangaza hatua ya Serikali kukusudia kuzifutia usajili taasisi mbalimbali za kidini, endapo zitabainika kukiuka sheria ya vyama vya kijamii.

Chikawe akasema kinachofanywa na taasisi hizo ni kinyume cha sheria ya vyama vya kijamii Sura ya 337 na kanuni zake inayosimamia uendeshaji wa taasisi hizo.

“Kuanzia Aprili 20, mwaka huu taasisi zitakazoshindwa kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa fedha za mwaka pamoja na kulipa ada zao zitachukuliwa hatua,” akaeleza Chikawe.

“Viongozi wa taasisi hizi, wanapokutana na kutoa matamko yanayolenga kuwashawishi waumini wao wafuate maelekezo yao kuhusu masuala ya Katiba Inayopendekezwa au uchaguzi mkuu ujao, matamshi kama hayo yanakiuka sheria za usajili wa taasisi hizo,” anasema Chikawe.

Wachambuzi wanasemaje?

Dk Benson Bana anaeleza kuwa “Si vizuri kukataza watu kushiriki zoezi halali kisheria, aidha siyo vizuri kuanza kujenga tabia ya kushinikiza mamlaka halali kufanya uamuzi kukidhi matakwa ya vikundi shinikizi.”

Kwa mujibu wa Dk Bana ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, katika masuala ya utawala na siasa kufanya hivyo ni kujenga msingi mbaya kinyume na utawala bora.

Anasema Sheria ya Kura ya Maoni ipo wazi kwamba kambi zinazotakiwa ni inayoikubali mapendekezo yaliyopo na kambi inayoyakataa mapendekezo hayo. Kundi lolote linaruhusiwa kuhamasisha upande unaotaka

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...