Skip to main content

Kikwete awajibu walimu

RAIS Jakaya Kikwete amewajibu walimu kuwa katika kipindi cha miaka 10 ya uongozi wake amefanya kazi ya uboreshaji maslahi yao na kuahidi kumaliza madai yao yote kabla hajang’atuka madarakani Oktoba mwaka huu.

Kikwete alisema hayo alipokuwa akiwajibu walimu ambao waliandika bango kwenye maandamano ya sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani na kupita mbele yake na kusomeka kuwa ‘Shemeji Unatuachaje?’ ikiwa ni lugha ya utani kwa kuwa mke wake Mama Salma ni mwalimu.

Maandamano hayo yalifanyika katika Jiji la Mwanza ambapo Kikwete alikuwa mgeni rasmi. Katika majibu yake alisema ameboresha miundo ya utumishi katika sekta mbili za walimu na afya.

Aliwaambia walimu mambo aliyoyafanya ni kuanzishwa kwa Muswada wa Bodi ya taaluma ya walimu na Tume ya utumishi ya walimu lengo ni kuwasaidia, kuwainua pamoja, kuwaendeleza na kufanya kila kitu katika sekta hiyo.

Alisema maandalizi yake yameshakamilika bado kupelekwa bungeni. Alisema Bodi ya taaluma ya walimu itawaendeleza walimu kitaaluma.

Katika hotuba hiyo kwa wafanyakazi iliyotumia zaidi ya saa moja, Kikwete alisema anatumia nafasi hiyo kuwaaga ‘shemeji’ zake ambao ni walimu, kwani imebakiza muda mfupi amalize muda wake.

Alisema muundo wa walimu umeanza Julai mwaka jana wa kulipa malimbikizo yao lakini haukuenea katika maeneo yote kwa haraka, lakini mwaka mpya wa fedha jambo hilo litawekwa vizuri.

Alisema malimbikizo ya walimu 30,668 hivi sasa ni Sh 53,155,440,406 na walimu 29,143 wamelipwa Sh bil 25.223 huku madai ya walimu 7,668 ambayo ni Sh bilioni 9.2 yatalipwa mwaka mpya wa fedha.

Lakini baadhi ya madai hayo ya walimu 30,807 ya Sh bilioni 17.3 yamekutwa na dosari mbalimbali na kutaka yarudishwe ili halmashauri iyahakiki na yalipwe.

“Fanyeni hima dosari zikamilike walipwe. Baada ya kusema hayo nina uhakika ninawaacha vizuri,” alisema Rais Kikwete. Pia alielezea furaha yake ya uanzishwaji wa benki ya walimu, ambayo serikali inaiunga mkono na kutoa ushirikiano ili lengo la walimu litimie.

Akizungumzia kada ya uuguzi, Rais Kikwete alisema serikali ilibadilisha muundo mwaka 2010 ambao uliathiri baadhi ya wauguzi kwa kuwa viwango vyao vya mishahara vilishuka, hilo ni kosa.

“Nimeagiza warejeshewe mishahara yao ya awali na malimbikizo yalipwe,” alisema. Alisema katika kada hiyo mwaka 2010 watumishi 476,430 walipandishwa vyeo

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...