Skip to main content

Kikwete: "Nisingekuwa Rais Ningekuwa Msanii Mkali wa Bongo Fleva.".........HOTUBA Nzima ya Rais Kikwete Aliyoitoa Jana Mei Mosi Iko HAPA

RAIS Dkt. Jakaya Kikwete, ametamba kuwa angakuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya basi angelikuwa wa “BongoFleva” kutokana na kuwa na sauti nzuri yenye kumudu kuimba nyimbo kwa ufasaha zaidi.

Kauli hiyo aliitoa  jana jijini Mwanza kwenye uwanja wa michezo wa CCM Kirumba wakati wa maadhimisho ya kilele cha sherehe za Mei mosi zilizofanyika Kitaifa jijini Mwanza kwa mwaka huu wa mwisho wa utawala wake.

Dkt. Kikwete aliimba wimbo wa Bendi ya OSS (Ochestra Safari Sound) wenye mashairi yasemayo "Mimi msafiri bado niko njiani sijui lini nitafika... naulizia watu kule ninakokwenda....”  na kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi waliomshangilia ambapo alitamba kuwa na sauti ya mauzo.

“Mmesikia sauti yangu si mbaya sana,  hakika nisingekuwa Rais wa Nchi hii basi nigekuwa msanii wa bongo fleva kama akina Ali Kiba, Diamond na wasanii wengine wakali nikiuza album zangu kwani ningekuwa tishio  kwa kuimba...” alisema.

Rais pia alimpongeza msanii maarufu nchini wa kizazi kipya mwenye mashairi na misamiati ya maneno magumu, Mrisho Mpoto, kwa kumtaka kujibu bango la walimu lililokuwa na ujumbe uliosomeka “Shemeji Unatuachaje??” ambapo alijibu kwa kusema kuwa "kuoa mwalimu nitabu kweli kweli haya nimesikia."

Aliwapongeza viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) nchini kwa kumwalika Mpoto “Mjomba” .Mara nyingi amekuwa akitoa ujumbe mzito kupitia fani yake ya muziki na mashairi lakini yakifikisha ujumbe bara bara kwa wananchi katika sherehe mbalimbali za kitaifa na makongamano .

Hotuba

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Wananchi wanaopata maji wafikia 55%

Jumanne Maghembe. SERIKALI imesema kwamba sekta ya maji kwa kutumia mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) imeongeza wananchi wanaopata huduma ya maji kutoka milioni 15.2 Juni, 2013 hadi kufikia milioni 20.9 sawa na asilimia 55. Hata hivyo, baadhi ya wabunge na Kambi Rasmi ya Upinzani wamepinga takwimu hizo. Aidha wabunge waliozungumza baada ya bajeti kusomwa jana, wabunge hao walisema kwamba kuna udanganyifu mkubwa wa takwimu zilizowasilishwa ndani ya Bunge, huku Kambi ya Upinzani ikidiriki kusema kwamba mipango ya Serikali ya kuwapatia wananchi wake maji imeshindwa. Msemaji wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Maji, Mohamed Rajab Mbarouk alisema kwamba takwimu za utafiti wa kitaifa katika eneo la maji, zinaonesha kwa sasa wananchi wanaopata maji safi na salama ni asilimia 40 tu na sio asilimia 57.8 kama ilivyorekodiwa katika taarifa za Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (Mkukuta). Alisema takwimu nyingi pamoja na visima vinavyofanya kazi si sahihi, hali inayodhihi...