Skip to main content

Kocha: Simba ndio bingwa

BAADA ya Simba kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC juzi, Kocha wa timu hiyo, Goran Kopunovic licha ya kuiombea Yanga iifunge timu hiyo ya Chamazi, ametamba kuwa Simba ndio ‘mabingwa’ msimu huu.

Ushindi huo unaifanya Simba kutofautiana kwa pointi moja na Azam FC, ingawa wapinzani wao hao wana faida ya michezo miwili ambayo kama itashinda, itachukua nafasi ya pili wakati Simba imebakiza mchezo mmoja pekee.

Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 44, moja nyuma ya Azam FC, wakati wakiwania kumaliza nafasi ya pili nyuma ya bingwa mpya, Yanga na kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.

Akizungumza baada ya mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kopunovic alisema uwezekano wa kuchukua nafasi ya pili utategemea na matokeo ya mchezo wa Yanga na Azam FC utakaochezwa kesho.

“Hatima yetu ya kushika nafasi ya pili itategemea na mchezo wa Yanga, kwa hiyo tunasubiri tuone kwani tunatamani tushiriki michuano ya kimataifa mwakani,” alisema kocha huyo raia wa Serbia.

Akizungumzia mchezo huo dhidi ya Azam FC, Kopunovic alikisifu kikosi chake kwa kucheza vizuri na kufanikiwa kupata matokeo ambayo waliyataka.

Alisema kikosi chake kilionesha kuimarika kwani kila mchezaji aliyeingia alionesha juhudi ya kutaka kufanya vizuri. Licha ya kuiombea Azam FC ifungwe, kocha huyo alijitapa kuwa wao ndio mabingwa kwa vile walifanikiwa kuifunga Yanga na Azam msimu huu.

“Yanga wanasema wao ni bora na Azam vile vile, lakini niseme kuwa sisi ni bora kuliko wote kwa sababu tumewafunga, kwa hiyo tu naweza kusema ni mabingwa,” alitamba kocha huyo mwenye vituko akiwa uwanjani.

Katika Ligi Kuu msimu huu, Simba ilitoka sare ya bao 1-1 na Azam FC katika mzunguko wa kwanza kabla ya kushinda juzi, wakati Simba ilitoka sare ya 0-0 na Yanga katika mzunguko wa kwanza kabla ya vijana wa Jangwani kuzama kwa bao 1-0 katika marudiano, katika mechi ya kwanza ya Kopunovic akiwa na Simba.

Kocha huyo wa Simba hakusita kuipongeza Yanga kwa hatua waliyofika kwanza katika kuchukua ubingwa wa ligi, lakini pia kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Alisema Yanga walionesha mchezo mzuri dhidi ya Etoile Sportive du Sahel kwani walijitahidi kwa uwezo wao.

Naye Kocha wa Azam FC, George Nsimbe alisema hawaangalii nyuma walipofungwa, kwani wanajipanga kwa mchezo dhidi ya Yanga ili kuondoka na pointi tatu.

Inahitaji pointi tatu kuifuta Simba kupanda ndege mwakani. Nsimbe alionesha matumaini kuwa iwapo watajitahidi katika mchezo huo watachukua nafasi ya pili.

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...