KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam, Hans van der Pluijm ametangaza kikosi chake bora cha wachezaji 11.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali, kocha huyo golini atamweka Ally Mustafa, akidhani kuwa ndiye aliyecheza vizuri zaidi katika nafasi hiyo wakati beki wa kulia ni pamoja Juma Abdul wakati mabeki wa katikati ni Paschal Wawa na Nadir Haroub.
Mabeki wa kushoto ni Tshabalala kutoka Simba, ambaye alisema hajui jina lake halisi.
“Safu ya kiungo ni Said Ndemla kutoka Simba, winga ya kulia ni Msuva, winga wa kushoto Emmanuel Okwi, kiungo cha mbele Niyonzima na washambuliaji wawili ni Amissi Tambwe na Kavumbagu’. “Sikuwepo wakati ligi inaanza, nilianza kazi Yanga mwishoni mwa Desemba mwaka jana, lakini kwa kipindi nilichoona ligi nimewaona wachezaji hao kuwa bora zaidi msimu huu,” alisema kocha huyo raia wa Uholanzi.
Kikosi na timu wanazotoka wachezaji hao ni kama ifuatavyo:- Ally Mustafa (Yanga) Juma Abdul (Yanga) Mohamed Hussein ‘Tshabala’ (Simba), Nadir Haroub (Yanga) Paschal Wawa (Azam FC) Said Ndemla (Simba) Simon Msuva (Yanga) Haruna Niyonzima (Yanga) Amiss Tambwe (Yanga) Didier Kavumbagu (Azam FC) Emmanuel Okwi (Simba).
Comments
Post a Comment