Skip to main content

Lawama kibao Tuzo za Muziki za KTMA

Mashabiki ambao ndiyo wapiga kura, bado wanajiuliza kwa nini majina ya wasanii kadhaa ambao walitamba, yamekosekana. Tatizo ni nini?
SHARE THIS STORY
0
inShare

Kuna majina ukikutana nayo katika orodha ya wateule wanaowania Tuzo za Muziki za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA), unaanza kuyalinganisha na yale maarufu yaliyong’ara mwaka 2014, lakini hayamo katika tuzo za mwaka huu.

Mashabiki ambao ndiyo wapiga kura, bado wanajiuliza kwa nini majina ya wasanii kadhaa ambao walitamba, yamekosekana. Tatizo ni nini?

Katika kipengele cha mwimbaji bora wa kiume wa bendi, majina yaliyoingia ni Jose Mara, Kalala Junior, Khalidi Chokoraa, Chaz Baba na Nyoshi El Sadat. Lakini bado mashabiki wanajiuliza ni kwanini jina la Christian Bella halikuingia wakati ndiye ambaye kwa mwaka mzima alifanya vitu vikubwa na nyimbo zake bado zinatamba.

Minong’ono iliyokuwapo ilidai kuwa Bella hafai kuwapo kwa waimbaji wa kundi kwa kuwa anasimama mwenyewe. Ukweli ni kwamba Bella yupo katika bendi ya Malaika na mara nyingi bendi hii imekuwa ikiitwa Christian Bella and Malaika Band na mwaka jana ilitamba na kibao cha “Nakuhitaji”.

Hata kama nyimbo nyingine alirekodi peke yake bila ya bendi ya Malaika, bado muziki wake ni wa bendi, inashangaza kwamba waandaaji wamelipuuza hilo. Kipengere kingine kilichozua maswali ni Mtunzi Bora wa Mwaka wa Bendi ambacho Bella pia ametemwa, licha ya kutunga nyimbo nyingi zilizokubalika kama “Nani Kama Mama” ambao hakuna ubishi kuwa una sifa zote za kuwa Wimbo Bora wa 2014. Badala yake wameingia akina Jose Mara, Nyoshi El Saadat, Rogart Hegga Katapila, Hussein Jumbe na Richard Mangustino, ambao wengi hawakuwa na kazi zozote mwaka jana.

Katika tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike wa Bendi, hakukuwa na wateule, lakini katika macho ya haraka kuna nyimbo kama “Kariakoo” wa Skylight Band ndani yake kuna mkono wa Aneth Kushaba. Ilishindikana nini kuwamo. Kuna wanamuziki kama Luiza Mbutu, Taji na wengineo ambao walifanya vizuri mwaka 2014.

Kwa upande wa Wimbo Bora wa Taarabu kulikuwa na nyimbo mbili pekee zilizopita ukiwamo wa “Hasid Hana Sababu” wa Hadija Yussuf na “Lady With Confidence” wa Khadija Kopa. Hili ni eneo ambalo lilikuwa na kazi nyingi zilizotamba pengine kazi ingekuwa ni kuzipunguza hadi zibakie tano.

Hii ni kwa mujibu wa jarida la Starehe, lakini wadau walikuwa na mengi ya kuelezea.

Josephat Kambi, mmoja wa mashabiki wa muziki, anauliza: “Katika upande wa tuzo za utunzi bora, sijajua ni vigezo gani vinavyotumika kwa kuwa wapo wasanii tunawajua hawawezi kutunga wimbo mzuri, ila kuna wasanii ambao wanatunga na kuimba. Mfano mzuri ni Barnabas. Kuna kila haja ya wasanii wetu wanapotoa wimbo wataje na mtunzi ili watunzi hawa washirikishwe pia kama kina Ude Ude wametunga nyimbo nyingi za Lady Jaydee, Ali Kiba na wengine.”

Wasanii

Mo Music amejitoa katika kinyang’anyiro hicho tangu wateule watangazwe Aprili.

“Nimeingia katika kipengele cha kuwania Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba wa mwaka, ilhali mimi ni msanii chipukizi majibu yake nimewekwa na vigogo kama kina Diamond, Lady Jaydee, Bella na wengineo,” alilalamika.

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...