Skip to main content

Mastaa wa kimataifa kutua Yanga 2016

KLABU ya Yanga imesema inatarajia kufanya usajili wa wachezaji wazuri wa kimataifa kwa ajili ya kukisaidia timu yao ya soka kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema wataangalia wachezaji wengine wazuri ambao watasaidia sio tu katika michuano ya kimataifa, bali ikiwezekana kutetea taji hilo kwa msimu ujao.

Muro alisema hawatarajii kufanya usajili wa wachezaji kutoka Simba kwani wamejifunza kutokana na makosa. “Usajili tutafanya kwa wachezaji wengine wa kimataifa hivyo hatutarajii uongozi wetu utasajili wachezaji kwa watani zetu Simba, hata kama ni mzuri kwa kiasi gani au ni malaika, hatutafanya wala hatutarajii,” alisisitiza Muro.

Kuhusu ni wachezaji gani wataachwa, alisema ni mapema kusema kwa sasa kwani hilo ni suala la benchi la ufundi. Alisema hajui ni nani ataachwa kwani hayo hujulikana baada ya kumalizika kwa msimu na kisha wakishapewa ripoti ya benchi hilo ndipo watajua wanaohitajika na wasiohitajika.

Mkuu huyo wa Habari pia alikanusha taarifa za usajili wa Simon Msuva na Haruna Niyonzima Simba kwamba ni za uzushi na kuwataka wanachama wa klabu hiyo kutosikiliza taarifa hizo.

Pamoja na hayo, alizungumzia mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Etoile Sportive du Sahel uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Sousse nchini Tunisia kuwa licha ya kutolewa, wamechukulia kama ni sehemu ya changamoto kujipanga kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa mwakani.

“Tumeyakubali matokeo, tumejifunza mambo mengi na tunachukulia mapungufu yetu kwa ajili ya kujipanga,” alisema. Yanga ilitolewa baada ya kufungwa bao 1-0 na hivyo kutupwa nje kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Aprili 18, mwaka huu.

Aidha, timu hiyo ya Jangwani tayari imetawazwa bingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya 25 baada ya kufikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine 13 zinazoshiriki ligi msimu huu. Leo inacheza na Azam FC

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...