Skip to main content

Mchakato wa urais Chadema kuanza Julai 20

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza tarehe za wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuchukua na kurejesha fomu, ambapo kwa nafasi ya Rais, zitatolewa Julai 20 na kurejeshwa Julai 25.

Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema jijini Dar es Salaam jana, tarehe hiyo na za madiwani na wabunge kuchukua fomu, zimepitishwa na Kamati Kuu ya CHADEMA kwenye mkutano uliofanyika kwa siku mbili.

Kwa mujibu wa Mbowe, wabunge wataruhusiwa kuanza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo kwa vipindi viwili tofauti, ambapo Mei 18 itakuwa siku ya watakaotaka kugombea Ubunge kwenye majimbo, ambayo kwa sasa chama hicho hakina wagombea.

Aidha, ilielezwa kuwa siku hiyo wanaowania nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum nao wataruhusiwa kuchukua fomu na kuzirejesha na wanaowania Ubunge kwenye majimbo yasiyo na wabunge wa CHADEMA ifikapo Juni 25.

“Julai 6 itakuwa ni siku ya kuchukua fomu za ubunge katika majimbo ambayo chama chetu kina wabunge na Julai 10 ndio zitatakiwa kurejeshwa”, Mbowe alisema na kuongeza kuwa, Mei 18 itakuwa siku ya kuchukua fomu za Udiwani kwenye Kata ambazo chama chake hakina Madiwani, zitakazotakiwa kurejeshwa Juni 25.

Kwa upande wa kata ambazo kuna madiwani wa chama hicho, imeelezwa kuwa, fomu za Udiwani zitaanza kutolewa Julai mosi na kurejeshwa Julai 10, kuruhusu uteuzi wa mwisho wa wagombea Udiwani na wale wa Viti Maalum.

Kutokana na ratiba iliyotolewa na chama hicho, uteuzi wa mwisho wa wagombea Ubunge utafanyika Agosti mosi na Agosti 2, wakati Baraza Kuu la Taifa la chama hicho litakaa Agosti 3 na Mkutano Mkuu kuendeshwa Agosti 4.

Mbali na hayo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alisema muungano wao na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), umeamua kutumia mkakati wa kuachiana nafasi katika maeneo ambayo mgombea anayependekezwa anaonekana kuyamudu ili kuishinda CCM.

Mjumbe wa Jopo la Wataalamu katika UKAWA ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Profesa Mwesiga Baregu alisema mkakati mwingine wanaoufikiria kuutekeleza hapo baadae ni wa kuifanya UKAWA iwe chama kimoja.

Wakati akijibu swali la gazeti hili kwenye mkutano na wanahabari alisema, “Wazo hilo tunalo lakini kwa sasa hatuwezi kuua vyama vyetu kwa kuwa bado tunajijenga, kuendelea kufahamiana na kuelewana”. “…Ikibidi hapo baadae, kabla ya uchaguzi mkuu, tutajiunga na kuwa chama kimoja tu, yaani UKAWA bila CHADEMA, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF,” alisema

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...