Skip to main content

Mkurugenzi Mkuu Vodacom aliyejiuzulu Aula Qatar ......Mitandao Yahusisha Kujiuzulu Kwake na Kashfa ya Upotevu wa Bilioni 700 za Kitanzania

Aliyekuwa  Mkurugenzi  mkuu  wa  Vodacom  aliyejiuzulu hivi  karibuni  Rene Meza amepata shavu katika kampuni nyingine ya mawasiliano  nchini Qatar ijulikayo kama Ooredoo Mynmar kuwa Mwenyekiti  mtendaji  wa tawi la Mynmar.

Aidha, taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana  na kampuni hiyo imesema kwamba Rene Meza atachukua nafasi ya  Ross Cormack ambaye anatarajiwa kuachia nafasi hiyo mwaka huu.

Kwa mujibu wa mtandao wa Afrika Kusini umebanisha kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom amejiuzulu  ili kufanya kazi nyingine.

Hata hivyo mitandao ya kijamii  mbalimbali  nchini Tanzania imehusisha  kuondoka kwake  na kashfa ya upotevu wa takribani  bilioni 700 fedha za kitanzania ambazo ni sawa dola za Kimarekani  milioni 350.

Taarifa  hizo  zinaarifu  kuwa  bwana Meza alikuwa kwenye  ‘kitimoto’ cha maofisa wa juu wa Kampuni hiyo akihusishwa na kashfa ya kupokea dola milioni 5 kutoka kwa Mmiliki wa Shivacom,Tanil Somaiya ambaye  alimpa  ili  kumziba mdomo   kutokana  na  kashfa   ya  uzalishaji, usambazaji na uuzaji  wa  vocha  bandia  zilizokuwa  zinajulikana  kwa  jina  la  "Jero jero".

Rene Meza alijiunga na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom mwaka 2011 akitokea kampuni ya Bhati Airtel Ltd ya nchini Kenya.

Ifuatayo  ni taarifa iliyotolewa na kampuni ya Ooredoo Mynmar ya nchini Qatar

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...