a Gratian Mukoba.
MCHUANO mkali umeibuka ndani ya Chama cha Walimu Nchini (CWT) baada ya wagombea 28 kujitosa kuwania Urais wa chama hicho chenye nguvu kutokana na kuundwa na idadi kubwa ya watumishi wa umma.
Miongoni mwa wanaogombea ni rais wa sasa wa chama hicho, Gratian Mukoba ambaye pia Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA).
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Alhamisi wiki hii kwenye Ukumbi wa hoteli ya Ngurdoto, Arumeru mkoani Arusha siku ambayo itakuwa inahitimisha mkutano mkuu wa siku tatu wa chama hicho unaotarajiwa kufunguliwa kesho na Rais Jakata Kikwete.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, Kanda ya Ziwa imeongoza kwa kutoa wagombea wengi wakiwemo wa mkoa wa Mwanza, Kaliyaya Masunga wa Ilemela, Magesa Kirati wa Kwimba, Marwa D. Marwa wa Nyamagana na Mashauri Benedict kutoka Sengerema.
Wengine wa Kanda ya Ziwa ni Charles George wa Geita, Godi Kiduma, Lyangombe Dotto na Malimi Macheyeki kutoka Maswa mkoani Simiyu na Juma Boniface wa Bunda, mkoani Mara.
Pia yuko Odeka Samson wa Musoma (Mara). Kutoka Dar es Salaam, Mukoba (Ilala) anawaongoza wagombea kutoka mkoa huo, wengine wakiwa Midelo Mathias wa Kinondoni, Rwebangira Anderson wa Temeke na Maguye Charles wa Mkoa wa Pwani.
Mkoa wa Morogoro una wagombea wawili ambao ni Asumbisye Frank na Senyagwa Daudi, kutoka Dodoma ni Ambakisye Fadhili na Iringa ina mgombea mmoja Seugali Luth Saida, wakati Mbeya imetoa mgombea kutoka Rungwe, Canon Mtewe Leonard. Wengine ni Christopher Banda kutoka Mtwara na Said Waninga kutoka Lindi.
Aidha, Arusha ambao ni mwenyeji wa Mkutano huo wa CWT ina mgombea mmoja tu, Laizer Miage anayetoka wilayani Karatu. Idadi kama hiyo, yaani wagombea 28, pia wanawania nafasi za Makamu wa Rais na katika kitengo hicho, wengi ni wale wanaotokea mkoa wa Dar es Salaam (5) na Kanda ya Ziwa (4).
Tisa wamejitokeza kuwania ukatibu mkuu na wengi ni kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo, Fredy Mbuguni, Nyamwero Bwire na Byarugaba Bandiho wote wa Mara, Zacharia Muganda wa Sengerema, Mwanza, na Edward Philipo wa Shinyanga.
Wengine ni Elisante Dyamyeku wa Morogoro, Yahya Msulwa wa Kinondoni, Dar es Salaam ambaye ni katibu Mkuu wa chama hicho na Meruma Wasato wa Kibaha, Pwani.
Wanaowania nafasi ya Naibu Katibu Mkuu, Ezekiel Oluoch na Mpumbe Joseph, wote kutoka Kinondoni Dar es Salaam. Wengine ni Kauka Akyoo na Augustino Daudi kutoka Hai, Kilimanjaro, Augustina Massawe wa Moshi, John Gadiye, Anthony Gamba, Mukangara James, na Wilson David hawa ni kutoka Mwanza.
Pia wamo Frank Chalamila wa Morogoro, Mayo Wilhelmon wa Manyara, Festo Moshi wa Mbeya, Prosper Mutungi, na Tangatya Santuce wa Dodoma, Michael Ndangwe wa Iringa, Shiku Peter, Marwa Mbeu wa Mara. Halafu Addallah Khalfani na Ismail A. Ismail wa Mtwara.
Wengine ni Kanyaiyangiro Evordius, Mathias Midelo na Fidelis Kisukilo kutoka Pwani, Lenda Majebera wa Tabora na Jairos Leonora wa Sumbawanga Rukwa. Pia wamo Raphael Joseph wa Geita na Simu Mussa wa Singida.
Comments
Post a Comment