Skip to main content

Msuva aitwa Taifa Stars

KINARA wa ufungaji Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na mshambuliaji hatari wa Mabingwa wapya wa ligi hiyo, Yanga, Simon Msuva ni miongoni mwa wachezaji 28 watakaoingia kambini Jumatatu kujiandaa na michuano ya Baraza la Vyama vya Soka Kusini mwa Afrika (COSAFA) inayoanza Mei 17, mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Msuva ambaye ameitwa kwa mara ya kwanza pamoja na chipukizi wa Simba Ibrahim Ajib, wamekuwa na kiwango kizuri msimu huu, huku wachezaji wawili wa kulipwa, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wakikosekana kutokana na kufuzu kwa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuzu hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wachezaji walioitwa ni timu zao katika mabano ni Deogratius Munishi (Yanga), Aishi Manula, Mwadini Ally, Shomari Kapombe (wote Azam FC), Kelvin Yondani, Nadir Haroub (wote Yanga), Abdi Banda (Simba), Oscar Joshua (Yanga), Aggrey Morris (Azam FC), Isihaka Hassan (Simba) na Salim Mbonde (Mtibwa Sugar).

Wengine ni Erasto Nyoni, Amri Kiemba na Salum Abubakar (wote Azam FC), Said Juma Makapu (Yanga), Frank Domayo (Azam FC), Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haruna Chanongo (Simba), Mwinyi Kazimoto (Al-Makhiya, Qatar), Simon Msuva, Salum Telela (wote Yanga), Ajib, Mrisho Ngassa (Yanga), John Bocco (Azam FC), Juma Luizio (Zesco United), Mwinyi Haji (KMKM) na Kelvin Friday (Azam FC).

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam, Nooij alisema ni lazima wachezaji wote waliotajwa hata kama ni majeruhi, wafike kambini kwenye Hoteli ya Tansoma kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.

“Tunatawaka wachezaji wote wafike siku hiyo, watafanyiwa vipimowale watakaobainika ni majeruhi watabaki na kwa ajili ya matibabu kisha watasubiri mechi nyingine za Afrika,” alisema kocha huyo raia wa Uholanzi.

Nooij alisema kati ya wachezaji hao 28, 20 tu ndio watachaguliwa kwenda Afrika Kusini na wanane watabaki Dar es Salaam, na kwamba ikitokea baadhi wakaumia, waliobaki ndio watasafirishwa kuziba pengo, lakini kama sivyo, basi watasubiri kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Afrika na ile ya Wachezaji wa Ndani (CHAN).

Alisema kwa vile ligi bado inaendelea iwapo ikimalizika kuna ambao wataongezwa baada ya kumalizika kwa msimu kwa ajili ya michuano hiyo mingine ya Afrika.

Naye Mratibu wa Taifa Stars, Martin Chacha alisema katika michuano hiyo ya Cosafa itakayochezwa katika Jimbo la Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, Stars inatarajiwa kucheza Mei 18, dhidi ya Swaziland na siku inayofuata dhidi ya Madagascar na kisha Lesotho.

Alisema wachezaji hao wataondoka Jumatano saa moja usiku kwa ndege ya Fastjet. Chacha alisema timu ikirudi kwenye mashindano hayo, itajiandaa tena kwa michuano ya Afrika dhidi ya Misri na CHAN ambapo inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Uganda mwezi ujao

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...