Skip to main content

Muhimbili Yakumbwa na Uhaba wa Damu

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imekumbwa na uhaba wa damu hali ambayo imeulazimu uongozi wa hospitali hiyo kuomba msaada wa dharura kwa Serikali na watu binafsi.

Uongozi huo pia umewaomba Watanzania, mashirika ya umma, makampuni  na watu binafsi kujitokeza kusaidia kuchangia damu  kuokoa maisha ya wagonjwa  wanaopelekwa katika hospitali hiyo.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha, ilieleza kuwa kwa siku hospitali hiyo huhitaji wastani wa chupa za damu 70 hadi 100 kwa siku.

Alisema hali hiyo inachangiwa na ongezeko la mahitaji ya damu ambayo hutumika zaidi hasa kwa wagonjwa wa dharura, kina mama wajawazito, wagonjwa waliofanyiwa upasuaji, watoto  na wagonjwa wa saratani.

“Kila mgonjwa wa upasuaji wa moyo anahitaji kiasi cha chupa tano mpaka sita za damu. Matumizi haya yanafanyika kabla, wakati na baada ya kufanyiwa upasuaji,” alisema Aligaesha.

Alisema kwa wiki hii wamelazimika kufungua kambi maalumu za Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka nchi mbalimbali ambao wanashirikiana na madaktari wa hapa nchini kufanya upasuaji wa moyo, kati ya wagonjwa watano hadi sita kwa siku.

“Wagonjwa wa moyo pekee huitaji chupa 30 hadi 36 kwa siku. Kambi hizi zimeanza mapema Aprili mwaka huu na tunatarajia kuwa nazo katika  miezi mitatu ijayo kama njia ya kuwafanya madaktari hawa waendelee kuja na kufanya upasuaji wa moyo kwa ufanisi  ambako damu huhitajika zaidi,” alisema Eligaesha.

Alisema hospitali hiyo ya taifa hutegemea kupata damu kutoka vyanzo vikuu viwili ambavyo ni ndani ya hospitali na  Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS).

“Makusanyo ya damu kutoka vyanzo vya ndani ni kati ya chupa 20 hadi 40 kwa siku  huku matumizi yakiwa chupa 70 hadi 100.

“Mathalani kuanzia Aprili 17 mwaka huu hatukuweza kupata damu hata chupa moja kutoka Mpango wa Taifa Damu Salama hali iliyosababisha upungufu mkubwa wa damu hospitalini hapa ikilinganishwa na mahitaji,” alisema.

Alisema Hospitali ya Taifa Muhimbili imejipanga kupitia kitengo chake cha Uchangiaji Damu kilichopo Maabara Kuu kuwapokea watu watakaojitokeza kuchangia damu.

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...