Skip to main content

Polisi Wapambana na Wananchi Njombe

JESHI la Polisi jana lililazimika kutumia zaidi ya saa 5.00 kupambana na wananchi waliokuwa wakiandamana bila kibali wakitaka kuchukua maiti ya mmoja wa wakazi wa Njombe aliyedaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi hilo wakati wa msako wa wanywa pombe.

Mtu huyo   inaelezwa alifariki dunia  juzi na mwili wake kuhifadhiwa katika  Hospitali ya  Kibena.

Inaelezwa wananchi hao walikuwa wakiandamana  kuuchukua mwili wa marehemu huyo na kuupeleka polisi.

Wakizungumzaia tukio hilo, baadhi ya wananchi walisema   juzi saa 3.00 usiku  polisi walivamia   kilabu  cha  pombe  kilichopo  Zenge Mtaa wa Kambarage na  kuwakamata  watu zaidi ya 20  waliokuwa wakilewa kilabuni hapo.

Baada ya  wananchi hao  kukamatwa  wakiwamo  wahudumu,  inadaiwa  polisi hao waliokuwa wamevalia ‘kininja’ waliwapiga  raia  walioonyesha  kukaidi agizo la  kutaka kutoa fedha walizokuwa nazo kama faini ya  kunywa  pombe   usiku huo.

Kijana mmoja,   Bashiri Mwalongo, ambaye alikuwa akitaka akitaka kutoka mlangoni alijikuta akipigwa na  kitu  kinachosadikika kuwa   risasi  tumboni  na  kufa papo hapo.

Inaelezwa kuwa  Polisi wa Kikosi  cha Kutuliza Ghasia (FFU), jana  walilazimika kuwatawanya waandamanaji hao kwa mabomu ya machozi.

Wananchi hao  walikuwa wanataka kwenda kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi,  kuwasilisha malalamiko yao.

Vurugu hizo   zilisambaa na kusababisha baadhi ya shughuli za jamii yakiwamo  maduka mjini Njombe kufungwa.

Mashuhuda walisema vurugu hizo zilisababisha barabata Kuu ya Njombe - Ruvuma na  Iringa ya  Njombe - Iringa na Njombe  - Makete  kufungwa na  waandamanaji hao ambao  walichoma  matairi ya magari katikati ya barabara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, alishindwa  kuzungumza na waandishi wa habari   kutoa ufafanuzi wa vurugu hizo kwa vile alichukua muda mrefu kwa kuwa katika  kikao na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...