Skip to main content

Rais Kikwete Kufungua Mkutano wa Mpango wa Uendeshaji

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
RAIS Jakaya Kikwete, leo anatarajiwa anatarajia kufungua mkutano wa Kanda ya Afrika kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa  Shughuli za Serikali kwa uwazi (OGP).

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam jana ilieleza kuwa kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Utawala Bora Unaozingatia Uwajibikaji na Uwazi” utafanyika Mei 20 hadi 21, mwaka huu katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Dhumuni la  mkutano huo ni kuleta ufanisi katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya uwajibikaji na utawala wa Serikali ili kutoa mrejesho kwa wananchi pamoja na uwazi kuhusu masuala ya ardhi.

“Kupata uzoefu wa utekelezaji wa OGP kutoka nchi wanachama katika bara la Afrika nan je ya Afrika kama vile taarifa za uwazi zinazoimarisha uwajibikaji” ilieleza taarifa hiyo.

Mkutano huo ni wa kwanza kufanyika nchini na wa pili kwa Kanda ya Afrika ambapo kwa mara ya kwanza  ulifanyika nchini Mombasa nchini Kenya mwaka 2013.

Mkutano huo unatarajiwa kuwa na washiriki 200 kutoka Serikalini, Asasi za kirai, Washirika wa Maendeleo wakiwemo Mawaziri kutoka ndani na nje ya nchi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa baadhi ya Taasisi za Serikali, wawakilishi kutoka Nchi wanachana wa OGP kutoka bara la Afrika.

Washiriki wengine ni kutoka nchi za Botswana, Zambia, Uganda, Marekani, Zimbabwe pamoja na washirika wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia, UNDP, UNICEF, UNESCO, MCC, USAID, DFID na JICA.

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...