Skip to main content

Serikali kumchunguza DC wa Karagwe

SERIKALI imepokea tuhuma dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Darry Rwegasira za madai ya kuwanyanyasa wananchi wa wilaya hiyo na kuwapa kipaumbele wahamiaji haramu kutoka Rwanda.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri MKuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenista Mhagama alisema hayo jana wakati akitoa kauli ya serikali kuhusu tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes (CCM) katika kikao cha bunge kinachoendelea.

“Hizi tuhuma sio za kupuuzia, ni tuhuma nzito, serikali tumelichukua hilo na tunalifanyia kazi ili kupata ukweli wake ili hatua stahiki zichukuliwe”, alisema Mhagama.

Awali akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa mwaka 2015/16, mbunge huyo alimtuhumu Mkuu huyo wa Wilaya kuwa ndiye anayechochea mgogoro wa ardhi katika wilaya hiyo, kwa kuwanyanyasa wananchi wa Karagwe na kuwapa kipaumbele wahamiaji haramu wa Rwanda.

“Migogoro mingi ya ardhi kwenye wilaya yetu inachangiwa na huyu mkuu wa wilaya, kwanza kimwili yuko Tanzania lakini kiroho yuko Rwanda, haiwezekani anawanyanyasa wananchi wa Tanzania kwenye ardhi yao na kuwapa kipaumbele wahamiaji haramu wa Rwanda,” alihoji Blandes.

Kutokana na hali hiyo, Blandes alimuomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kumshauri Rais Jakaya Kikwete kumwondoa mkuu huyo wa wilaya haraka wilayani humo.

Hata hivyo, baada ya mbunge huyo (Blandes) kumaliza kuchangia hakuna mtendaji wa serikali aliyejibu kauli hiyo, hadi kipindi cha uchangiaji kilipokamilika mchana kwa Mbunge wa Viti Maalumu, Rosemary Kirigini (CCM), kusimama na kuomba mwongozo kuhusu kauli hiyo.

“Mheshimiwa mwenyekiti, nimesimama hapa kwa Kanuni za Bunge ya 68(7) inayosema Mbunge anaweza kusimama muda wowote kutolea ufafanuzi, jambo lililojitokeza mapema wakati wa mjadala... sasa mheshimiwa mwenyekiti kuna tuhuma nzito zimetolewa leo (jana) hapa na Mbunge Blandes dhidi ya mkuu wa wilaya ya Karagwe,” alisema Kirigini.

Kirigini, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu alisema: “Tujuavyo sisi, Mkuu wa Wilaya ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Wilaya na ni Mwakilishi wa Rais kule, lakini kauli iliyotolewa hapa mbele yako ni ya uchochezi, sasa mheshimiwa mwenyekiti naomba mwongozo wako.”

Mara baada ya kumaliza, alisimama Mhagama na kusema: “Mheshimiwa mwenyekiti sisi kama serikali tumelichukua hili na tutafanya uchunguzi kuona alichokisema mheshimiwa (Blandes) na uhalisia na tutachukua uamuzi.”

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...