Skip to main content

Serikali Yapewa Mbinu Kujikimu Katika Bajeti

WAKATI Tanzania ikiwa imeshindwa kutekeleza Malengo ya Milenia wadau wa uchumi wametoa mbinu za kujikimu katika bajeti badala ya kutegemea nchi wahisani.

Malengo manane ya Milenia  ni pamoja na suala la kuondoa umasikini na njaa, elimu ya msingi kwa wote, usawa wa jinsia, kuzuia vifo vya watoto, afya ya uzazi, kupambana na Ukimwi, malaria na magonjwa mengineyo.

Akizungumza katika mkutano kuhusu Malengo ya Milenia, Dar es Salaam jana, Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Oswald Mashindano alisema miongoni mwa sababu za kutotekelezeka kwa malengo ya milennia ni ufinyu wa bajeti.

“Sababu kubwa ya kukosekana kwa rasilimali fedha ni tabia ya wafadhili kutotekeleza ahadi zao hasa asilimia 07 ya msaada wa maendeleo kwa nchi zinazoendelea (ODA),” alisema Dk. Mashindano.

Alisema badala ya kuendelekeza nchi wafadhili, Serikali inapaswa kuwa na vyanzo vingine ikiwa pamoja na vyanzo vya ndani.

“Kunatakiwa kuwe na chanzo kikuu cha fedha za maendeleo kama inavyoelezwa kwenye sera za taifa na mikakati ya maendeleo. Tuimarishe ushiriki wa sekta binafsi katika mikakati ya maendeleo katika ngazi za wilaya kama vile mipango ya wilaya na mipango ya uchumi na jamii,” alisema.

Alishauri pia kuimarishwa kwa mfumo wa kodi nchini kwa kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato hadi kwenye sekta zisizo rasmi.

“Kupambana na utoroshwaji wa fedha haramu nje ya nchi, ukwepaji wa kodi na rushwa, itasaidia. Inatakiwa pia kuongeza uwazi na kuhakikisha malipo yote ya Serikali yanakuwa wazi,” alisema.

“Tunatakiwa pia kuongeza faida kutoka katika sekta ya uchakataji kwa kutekeleza Mkakati wa Uwazi katika Sekta ya Uchakataji (EITI),” alisema

Awali akifungua mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Kuondoa Umasikini katika Wizara ya Fedha, Anna Mwasha alikiri Serikali kushindwa kutekeleza malengo yote ya millenia kwa kipindi cha miaka 15, akisema mikakati zaidi inafanyika.

“Wengi wetu tunatambua matokeo ya miaka 15 ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia tumeshindwa kutekeleza katika baadhi ya maeneo na inajulikana kama ‘biashara iliyoshindikana’,” alisema Mwasha.

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...