Skip to main content

Serikali yarudisha neema kwa wakulima Bumbuli Share bookmark Print Email Rating

mwanzo
Biashara

Biashara
Serikali yarudisha neema kwa wakulima Bumbuli
Share bookmark Print Email Rating

‘Mambo yote yako tayari. Kilichokuwa kinasubiriwa  ni kibali ambacho kimekwisha kutolewa na Rais Kikwete.’ January Makamba, Mbunge Bumbuli
Na Raisa Said, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Mei4  2015  saa 12:2 PM

Kwa ufupi

    Ni baada ya kuridhia kutoa fedha kwa ajili ya kifufua kiwanda cha chai

SHARE THIS STORY
0
inShare

Bumbuli. Mgogoro kati ya wakulima wa chai Bumbuli na mwekezaji wa Kiwanda cha Chai Mponde, umefikia tamati baada ya Serikali kuridhia kutoa fedha kwa ajili ya kufufua kiwanda hicho ambacho kilikuwa kimefungwa kwa muda wa miaka miwili baada ya wakulima kugomea kuuza majani mabichi ya chai katika kiwanda hicho.

Akizungumzia hatua ya kufufua uzalishaji wa kiwanda hicho kilichopo Mponde katika Halmashauri ya Bumbuli, Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba alisema, Serikali imeridhia kutoa Sh4 bilioni ambazo ni gharama za kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi, madeni ya malipo ya wakulima, ukarabati na mtaji wa kuanzia kuendesha shughuli za uzalishaji.

Mtaji huo utatumika pamoja na mambo mengine, kununua kuni za kwanza kwa ajili ya kiwanda na kukarabati magari ambayo alieleza kuwa baadhi  yake vipuri vilitolewa.

Makamba ambaye yupo katika ziara ya kutembelea jimbo lake la Bumbuli, alisema  Serikali ilituma wataalamu kufanya tathmini yenye lengo la kutambua gharama za ufufuaji wa kiwanda hicho kilichokuwa kikiendeshwa na Chama cha Wakulima wa Chai cha Usambara (Utega) na mwekezaji ambaye ni Kampuni ya Chai ya Lushoto katika miaka ya 2000.

“Hivi sasa ni Hazina ndiyo inayosubiriwa itoe fedha hizo kwa ajili ya kukarabati kiwanda na gharama nyingine,” alisema Makamba wakati akizungumza na wakulima katika Kijiji cha Kweminyasa, katika Kata ya Mponde.

Taarifa za kutolewa kwa kibali cha fedha za kufufua kiwanda hicho zimepokelewa kwa furaha na wakulima ambao hata hivyo waliiomba Serikali kuongeza kasi ya utoaji wa fedha ili waondokane na matatizo ya kiuchumi na kijamii yaliyotokana na kufungwa kwa kiwanda hicho.

Akizungumzia uamuzi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli, Beatrice Msomisi alisema,  Serikali imewapa matumaini ya kuongeza mapato ya ndani  yaliyodorora kutokana na kufungwa kwa kiwanda hicho.

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...