Skip to main content

Tanesco kuja na viwango vipya

Published on Thursday, 14 May 2015 00:07
Written by Sifa Lubasi, Dodoma
Hits: 783

SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) linakusudia kupanga viwango vipya vya malipo ya umeme vitakavyotoa unafuu kwa taasisi hiyo na wadau wake endapo vyombo vinavyohusika, ikiwamo EWURA vitaidhinisha.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Idara ya Mipango Mikakati kutoka Tanesco Makao Makuu, Patrick Sankara katika Mkutano ulioandaliwa na Tanesco Makao Makuu na kufanyika Dodoma mkoani hapa.

Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano ya shirika hilo na wateja wake wenye lengo la kupata maoni ya watumiaji wake na kuzijua changamoto zitakazokuwepo baada ya Tanesco, kuanzia mpango wa kugawa viwango vya bei ya umeme kulingana na muda wa matumizi.

Alisema wale watakaokubadili muda wa matumizi watapatiwa punguzo maalumu kwenye viwango vyao.

Alisema matumizi ya umeme kwa sasa hupanda ghafla kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 4:00 usiku na kusababisha msukumo wa umeme kutoka katika vyanzo vyake kupungua na kusababisha Tanesco kuwasha mashine za ziada kufidia mzigo huo.

Akiwasilisha mada katika mkutano huo iliyohusu “Viwango vya muda wa matumizi ya Umeme”, Sankara alisema kutokana mahitaji hayo Tanesco inaingia gharama kubwa kuhakikisha inakidhi matakwa ya wateja wake.

“Gharama zote za kufidia matumizi haya ya ziada ni za Tanesco hivyo tunadhamiria kuja na mpango wa kuwashawishi wateja wakubwa kuhamisha muda wa matumizi yao kutoka saa za jioni na kuja muda wa asubuhi na mchana ambapo matumizi si makubwa sana,” alisema.

Akichangia katika majadiliano hayo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa aliishauri Tanesco Mkoa wa Dodoma, kubuni utaratibu mpya wa kuwahudumia wateja wake ili kupunguza malalamiko na kukuza mahusiano mema.

Naye Kaimu Meneja wa Tanesco Kanda ya Kati, Joel Kuandika aliuambia mkutano huo kuwa wamepokea mapendekezo ya wateja hao na kuahidi kuyashughulikia ipasavyo.

Wakichangia mada hizo, baadhi ya watumiaji hao wakubwa walikubaliana na Tanesco kuhusu utaratibu mpya, lakini baadhi yao walionesha wasiwasi endapo Tanesco itaweza kusimamia utekelezaji wake kwa haki na umakini

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...