Skip to main content

Tanzania, Uganda Kutatua Migogoro Mipakani

SERIKALI za Tanzania na Uganda zimepiga marufuku watu kujenga nyumba katika mipaka inayozitenganisha nchi hizo ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima.

Agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki mkoani Kagera na wakuu wa wilaya za Misenyi kutoka Tanzania pamoja na wakuu wa Wilaya za Rakai na Isingiro za nchini Uganda.

Wakuu hao wa wilaya walitoa maagizo hayo baada ya kukutana kwenye mkutano wa ujirani mwema uliofanyika eneo la Mutukula, Tanzania.

Katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Fadhili Nkurlu, ambaye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo, alisema ajenda kuu katika mkutano wao ilikuwa ni kujadili jinsi ya kutatua kero mbalimbali, zikiwamo mfereji uliochimbwa katikati ya mpaka wa kimataifa katika eneo la Mutukula.

“Mfereji huo humwaga maji machafu kutoka upande wa Uganda na kuishia katika makazi ya Watanzania na unasababisha uharibifu wa mali na miundombinu mbalimbali.

“Katika suala hilo, tulikubaliana kuwa, suala hilo lirudishwe kwa wataalamu wa ardhi wa nchi husika ili walitazame kwa makini na kutoa ushauri na mapendekezo yatakayotatua kero hiyo.

“Wataalamu hao tumewapa muda wa siku 30 kuanzia Mei 7 mwaka huu ili wakamilishe jambo hili na kupeleka ripoti kwetu ili ufumbuzi upatikane.

“Wataalamu hao watazunguka mpaka mzima kuanzia jiwe namba 27 hadi 41 ili kubaini matatizo madogo madogo yanayosababishwa na jamii au yanayoikumba jamii iliyoko mipakani ili tuyafanyie kazi na kuendeleza amani iliyopo,” alisema Nkurlu.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Rakai, Mubiru Charles na Mkuu wa Wilaya ya Isingiro, Muhangi Herbert, walisema kwa nyakati tofauti kwamba wanasubiri ripoti itakayoletwa na wataalamu hao wa ardhi  ili kuona makosa yamefanyika wapi na yatafutiwe ufumbuzi

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...