SEKRETARIETI ya Mkoa wa Shinyanga imetumia Sh milioni tatu kununua mafuta ya magari wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani humo, bila kuwapo nyaraka zinazoonyesha matumizi hayo.
Hayo yalibainika jana katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na viongozi wa Mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Rubanzibwa Prejectus.
Prejectus alikiri kuwapo upungufu huo akidai walifuatilia bila mafanikio kutokana na magari waliyotumika kukosa rekodi za safari na mafuta yaliyotumika.
Kwa majibu hayo, Mjumbe wa Kamati hiyo na ambaye pia ni Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy (CCM), alipinga hatua hiyo akisema kitendo cha kuendelea na mbio za Mwenge ni sawa na matumizi mabaya ya fedha za umma.
“Haya mambo ya Mwenge yanatupotezea fedha tu…huu Mwenge unaleta matatizo tu,” alisema Keissy.
Hata hivyo, Kaimu Mwenyekiti wa PAC, Gaudence Kayombo, kila wakati alikuwa akimtuliza mbunge huyo kwa kumtaka kujadili hoja ya kukosekana nyaraka za uthibisho kuhusu matumizi ya fedha za mafuta.
Pamoja na hali hiyo wajumbe hao walibaini viongozi wa Mkoa wa Shinyanga wamekuwa na tabia ya kutumia fedha kwa shughuli ambazo ni tofauti na zile zilizokusudiwa ambako kwa mwaka 2011/12 zilitumika Sh milioni 24 na mwaka uliofuta Sh milioni sita.
Kwa majibu hayo kamati hiyo ya Bunge iliagiza sekretarieti ya mkoa huo kupeleka taarifa zilizokosekana za matumizi ya fedha hizo kuepuka kutumia fedha kwa matumizi tofauti na yale yaliyoelekezwa kwenye bajeti, kudhibiti matumizi ya magari.
Pia iliagizwa ipeleke taarifa zinazohitajika na kamati kabla ya Mei 14mwaka huu mjini Dodoma
Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania
Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati Mapinduzi hayo yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada ya tangazo la kupindulikwa kwake, Rais huyo alipanda ndege kurejea nchini kwake licha ya tangazo la kufungwa kwa mipaka yote na viwanja vya...
Comments
Post a Comment