Skip to main content

Tuesday, May 5, 2015 Sophia Simba: Rais Kikwete Bado HAJASAINI Muswada wa Sheria ya Mtandao, lakini Atausaini Muda si Mrefu

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kulia), akikata utepe kuzindua rasmi Taasisi ya maendeleo ya jamii ya Sitti Tanzania Foundation iliyofanyika Dar es Salaam juzi (kushoto) ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Sitti Mtemvu.

Na Mwandishi Wetu, Mpekuzi-Dar es Salaam
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, amesema kuwa kutokana na hali ya nchi kwa sasa Rais Jakaya Kikwete, atasaini sheria ya mtandao.

Kauli hiyo aliitoa jana  baada ya kuripotiwa na gazeti moja la kila siku mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa Kitabu cha Chozi la Sitti, ambapo alinukuliwa akisema kuwa Rais Kikwete ameshasaini sheria hiyo.

Akikanusha taarifa hiyo alisema kuna uwezekano amenukuliwa vibaya ila usahihi wa kile alichosema ni kwamba Rais ataisaini sheria hiyo kutokana na hali ya usalama wa nchi kwa sasa.

“Nilishosema si kwamba sheria imesainiwa, maana kwa mujibu wa utaratibu wa sheria ni kwamba sheria yoyote rais akishaisaini inapelekwa taarifa kwa Spika wa Bunge ambaye naye huitangaza.

“Kwa hiyo nami katika uzinduzi ule nilisema kama kukazia kauli ya Ikulu kuwa Rais Kikwete ataisani sheria ile kwani imefuata taratibu zote, ikiwemo kujadiliwa bungeni na hatimaye kuridhiwa.

“Hivyo ninawaomba Watanzania, waelewe kuwa hiki ndicho nilichokisema na si vinginevyo,” alisema Sophia.

Waziri huyo alisema pamoja na mitandao ya kijamii kusaidia kuleta maendeleo na kusambaza taarifa kwa muda mfupi, lakini kuna watu wamekuwa wakiitumia vibaya ikiwemo kuchafuana huku anayeathirika akishindwa kuchukua hatua za kisheria.

Pamoja hatua hiyo wadau wengi wamekuwa wakimshauri Rais Jakaya Kikwete asiisaini sheria ili kwani inaminya na hata kunyonga uhuru wa habari nchini.

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...