Skip to main content

Uchaguzi Yanga Julai

KLABU ya Yanga inatarajiwa kufanya uchaguzi Mkuu Julai 12 mwaka huu ambapo nafasi za Mwenyekiti , Makamu Mwenyekiti na Wajumbe zitawaniwa.

Awali uchaguzi huo ulikuwa ufanyike mwaka jana lakini baadhi ya wanachama walimwomba Mwenyekiti anayemaliza muda wake Yusuf Manji kuendelea kuwania tena nafasi hiyo kitu ambacho kilimlazimu kuwaomba wanachama hao asogeze mbele uchaguzi ili apate muda wa kufikiria ombi lao.

Akizungumza na gazeti hili Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga Francis Kaswahili, aliwataka watu mbalimbali wenye mapenzi ya dhati na klabu hiyo kujitokeza kuwania nafasi hizo kwa lengo la kuipa mafanikio zaidi klabu hiyo.

“Jambo hili ni la kikatiba na wala halina mjadala, tunataka Yanga iwe na viongozi ambao watatokana na utashi wa Wanayanga ni matumaini ya Kamati ya Uchaguzi kwamba hapatatoka mtu mwingine wa kutaka kuvunja misingi ya Katiba,”alisema Kaswahili.

Alisema lengo la kutangaza tarehe ya uchaguzi mapema ni kutaka kupata viongozi wapya ambao watapata muda mzuri wa kuiandaa timu kwa ajili ya kutetea ubingwa wao wa bara msimu ujao na kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa ambayo mwakani.

Kaswahili alisema fomu za kuwania uongozi kwenye klabu yao zitaanza kutolewa keshokutwa kwa kuzingatia taratibu na kanuni ambazo zitawekwa kwa nia njema ya kuhakikisha klabu yao inapata viongozi bora.

Mara ya mwisho Yanga ilifanya Uchaguzi wake Mkuu Julai 18,2010 ambapo Lloyd Nchunga alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Delvis Mosha alichaguliwa katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti huku wajumbe wakiwa ni Charles Mgondo, Ally Mayay, Mzee Yusuf na Theonest Rutashobolwa, Titus Ossoro, Sara Ramadhani, Mohamed Binda na Salum Rupia.

Lakini baadhi ya viongozi hao walijiuzulu nyadhifa zao na hivyo ikalazimika kufanyika uchaguzi mdogo Julai 15,2012 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee na Manji alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Clement Sanga akichaguliwa kama Makamu Mwenyekiti na nafasi za Wajumbe wakachaguliwa Aaron, Nyanda, George Manyama, Abdallah Bin Kleb na Valentine Katabalo

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...