Skip to main content

Vifo vya Watoto Kanisani kwa Gwajima Bado ni Utata.

MKAZI wa Mbezi Juu David Oturo, amesema yupo katika maandalizi ya kuwasafirisha watoto wake wawili  waliopoteza maisha  Mei 17 mwaka huu  baada ya kupigwa shoti ya Umeme   katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo katika Viwanja vya Tanganyika Peakas Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na jana baba mzazi wa watoto hao Oturo alisema kuwa anatarajia kuwasafirisha watoto wake ambao ni Sarah David(10) na Goodluck David(04) leo au kesho kuelekea Mkoani Musoma kwa ajili ya mazishi.

Alisema kifo cha watoto wake ni cha utata kutokana na kwamba watoto walikuwa ni wengi katika eneo hilo lakini ameshangaa watoto wake wote wawili kupigwa  na shoti ya umeme na wote baada ya hapo walipelekwa katika Hospitali ya TMJ na kuhamishiwa katika Hospitali ya Mwananyamala lakini wote walipoteza maisha.

Akizungumzia suala la ushiriki wa kanisa katika msiba huo alisema kuwa Askofu Gwajima pamoja na waumini wake wanafika nyumbani kwake lakini hawajashiriki kitu chochote.

“Kwa sasa nipo katika maandalizi ya kuwasafirisha watoto wangu kwenda Musoma kwa ajili ya mazishi, ingawaje katika maandalizi yangu  Askofu Gwajima na waumini wake hawajatoa kitu chochote kwa ajili yamaandalizi ya safari hii.

“Mimi ninachong’ang’ana  ni kuhakikisha kuwa wanangu ninawasafirisha kwenda kuwapumnzisha nyumbani kwetu nilipozaliwa ambako ni Musoma na si vinginevyo,” alisema  Oturo.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima alipotafutwa kuzungumzia swala hilo simu yake iliita bila kupokelewa na wakati mwingine ilikuwa ilikuwa haipatikani kabisa.

Pamoja na jitihada za kupiga simu kwa askofu huyo kugongwa mwamba, lakini ilisikika  miito ya nyimbo pamoja na mahubiri  mbalimbali katika simu yake.

Moja ya muito huo ulisikika ukisema  “Biblia ni njia kwa waliopotea, Biblia ni njia kwa waliokata tama, Biblia ni uponyaji kwa wagonjwa, Bibilia ni faraja kwa walio na dhiki,” yalisikika maneno hayo.

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...