Skip to main content

Vikao vizito vya CCM kuanza leo

na

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimejigamba kitatoka katika vikao vyake muhimu vya Kamati Kuu (CCM) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) vinavyoanza mjini hapa leo kikiwa imara kuliko hapo awali.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape Nnauye wakati akijibu swali kuhusiana na vikao vizito vya chama hicho vinavyoanza leo.

Nnauye alikuwa anaelezea maandalizi ya vikao vya kamati kuu kinachotarajia kuanza leo na halmashauri kuu ambayo itaanza kikao chake cha siku mbili kesho. Katibu huyo amesema wajumbe wa vikao hivyo ambavyo vitatoa mwelekeo wa sura ya uchaguzi itakavyokuwa ndani na nje ya chama hicho wameshaanza kuwasili mjini hapa.

Ajenda muhimu katika mikutano hiyo ni ratiba ya uchaguzi pamoja na kuwapata wagombea wa chama hicho ngazi zote. Ajenda nyingine ni hali ya kisiasa nchini na kutolewa kwa ratiba ya uchaguzi.

Pia vikao hivyo vinatarajia kutoa ratiba ya mchakato wa uchaguzi wa Urais na wagombea wengine, kutengeneza kanuni za kuwapata wagombea. Mambo mengine ni kupanga tarehe ya kuchukua fomu, kuzunguka kutafuta wadhamini na masuala mengine ambayo yanakigusa chama.

Mambo yanayotarajiwa kujadiliwa katika vikao hivyo ni pamoja na hatma ya makada wanaotaka kuwania kiti cha Urais ambao walitangaza nia kabla ya wakati na wakatolewa karipio na chama hicho cha kuwataka watulie na kusubiri muda mwafaka.

Tayari kamati ndogo ya Udhibiti na Nidhamu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake, Philip Mangula ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM -Taifa, imeshafanya vikao vyake mjini Dodoma kupitia taarifa za utekelezaji wa adhabu kwa makada sita wa chama hicho wanaodaiwa kuanza kampeni kuwania urais mwaka 2015 kabla ya wakati.

Makada hao waliozuiwa kujihusisha na kampeni kwa miezi 12, huku mienendo yao ya kisiasa ikifuatiliwa ni January Makamba, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

Mji wa Dodoma unaonekana kuwa shwari licha ya kuwa na pilikapilika nyingi na shauku ya wananchi ikiwa kubwa ili kufahamu yatakayojitokeza katika vikao hivyo.

Nje ya makao makuu ya CCM, wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali ikiwemo nguo za Chama wanaonekana kuongezeka huku maatarajio yao makuu yakiwa ni kufanya biashara

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...