Skip to main content

Viongozi Afrika watakiwa kuepusha nchi na migogoro

MWAKILISHI wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani, Balozi Amina Salum Ally amewataka viongozi wa Afrika kutumia mbinu mbalimbali ili kuziepusha nchi zao na migogoro ya mara kwa mara inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani na kudumaa kwa uchumi.

Aliyasema hayo katika mahojiano maalum na kituo cha televisheni cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Mlimani TV) juzi usiku alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali yanayohusu Bara la Afrika.

Alisema, baadhi ya nchi za Afrika zimekuwa katika wakati mgumu kukua kiuchumi kutokana na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe kitu ambacho mbali na kupoteza amani iliyopo, kinahatarisha pia kukua kwa uchumi kwa mataifa hayo.

Ally alisema uchumi wa taifa lolote lile hauwezi kustawi ikiwa viongozi wake watashindwa kusimamia hali ya utulivu na amani.

“Wawekezaji wanapenda kuonawanawekezaji vitega uchumi vyao katika mazingira yenye amani na utulivu. Aliongeza: “Inashangaza kuona baadhi ya nchi za kiafrika zimekuwa zikitumia muda mwingi katika mizozo ya wenyewe kwa wenyewe, hali hii haiwezi kuvutia wawekezaji jambo ambalo linaathiri ukuaji wa uchumi wa bara hili.”

Ally ambaye amebobea katika masuala ya kiuchumi alieleza kusikitishwa kwake na hali ilivyo katika nchi ya Burundi na kusema kuwa kinachotakiwa kufanyika katika mazingira ya nchi hiyo na nyingine zenye migogoro ni watu kukaa chini na kuzungumza kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kumaliza mizozo.

“Mimi naamini katika meza ya mazungumzo, ni kitu cha kawaida kuwa na mitazamo tofauti lakini mwisho wa siku ni vema kukubaliana kutokubaliana bila kumwaga damu ya mtu kwani siku zote mazungumzo ndiyo msingi wa taifa imara,” alisema

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...