Skip to main content

Vyama vya siasa vyakemewa kuhoji kipolisi

majukwaa yasiyo rasmi na kuhoji kipolisi mwanachama mmoja mmoja anayetuhumiwa kukosa, ni kichocheo cha uvunjifu wa amani, hivyo ikemewe, imeelezwa.

Mtaalamu wa masuala ya utatuzi wa migogoro ya kisiasa, Gharib Galant, aliyepewa kazi na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP), atafiti na kuishauri Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, juu ya njia bora za kutatua migogoro ya vyama vya siasa, ndiye aliyesema hivyo Dar es Salaam jana.

Akizungumza kwenye mkutano wa mashauriano kati ya vyama 22 vya siasa nchini, taasisi mbalimbali, wadau wengine wa siasa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa, kuhusu njia sahihi ya kusimamia na kuendesha kwa amani siasa za vyama vingi, katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu, Galant alisema, utatuzi wa migogoro unahitaji haki na uwazi.

Kwa mujibu wake, mwanachama anayetuhumiwa kukosa ndani ya chama, anapaswa kupewa nafasi ya kujieleza katika vikao rasmi apate hakiyake ya kujitetea na kutetewa pindi inapobidi, na si kuchukuliwa sehemu na wachache kwa maelezo ya kuhojiwa.

“Inapotokea mwanachama amepelekwa katika eneo fulani na kufanyiwa mambo yasiyostahili kwa taratibu zisizo rasmi nani atafahamu kuwa ametendewa haki au la? kila mmoja anaweza akatoka huko na kudai jambo lake...”.

“Hali hiyo inaweza kusababisha kuvunjika kwa amani ndani ya chama husika, mashabiki wa mwanachama anayekuwa amehojiwa na kudai kutotendewa haki, pamoja na makundi mengine ya jamii ambayo, kwa njia moja au nyingine yanakuwa yameguswa.

Mgogoro kama huo unapoibuka, athari yake inaweza kutingisha amani ya nchi,”alisema. Ingawa mtaalamu huyo hakukitaja chama chochote kuwa na tabia hiyo, Februari mwaka huu, Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kilituhumiwa kuwatumia walinzi wake, kumuadabisha aliyekuwa mlinzi wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa, Khalid Kagenzi kwa madai ya kutaka kumuua kiongozi huyo.

Kagenzi alilalamika kuwa walinzi hao walimkamata na kumfungia ndani ya chumba kimoja mali ya chama hicho, wakamtesa kwa kumpiga wakati wakimhoji kuhusu tuhuma hizo za kutaka kumuua Dk Slaa.

Pamoja na kuishauri ofisi hiyo ya Msajili wa vyama ikemee mapema hali hiyo, Galant alisema unapofanyika utatuzi wa migogoro ni lazima wahusika washirikishwe kwa ridhaa yao, wapewe nafasi sawa ya kujieleza bila kuwepo upendeleo kwa chama au kundi lolote.

Namna nyingine iliyotajwa na Galant kuwa ni bora katika kutatua migogoro ya vyama vya siasa au chama na wanachama wake ni ya kulipa Baraza la vyama vya siasa nafasi yake ya kutekeleza wajibu huo, badala ya kuikimbiza kwa Msajili au Mahakamani.

Katika hili, Galant alisema, “Ninashauri endapo Baraza hilo litashindwa kuwakutanisha wahusika wa mgogoro, au kuona kuwa mgogoro ni mkubwa unaoweza kuvuruga amani hivyo kusababisha uchaguzi mkuu na majukumu mengine makubwa katika nchi yasifanyike kwa wakati, litafute usaidizi wa wataalamu wa kutatua migogoro wanaokubalika ili wafanye kazi hiyo”.

Aliongeza kuwa kabla ya kuanza kupanga kushughulikia migogoro ni vizuri ukafanywa utafiti wa aina ya migogoro, ili kujua ni njia zipi zitumike kuimaliza, badala ya kukimbilia kuisuluhisha kwa sababu njia nyingine zinaweza kuizidisha.

Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula alipendekeza Baraza la Vyama vya Siasa nchini liwezeshwe kifedha lifanikishe kazi zake, ikiwa ni pamoja na kujisambaza katika ngazi zote, zikiwemo za chini.

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...