Mastaa wa Bongo Movies, Wema Sepetu, Vicent Kugosi ‘Ray’ na Hemmedy PHD wameshinda tuzo za TUZO ZA WATU za mwaka huu zilizofanyika usiku wa jana.
Wema sepetu ameshinda tuzo ya muigizaji wa kike anayependwa wakati Ray ameshinda tuzo ya muongozaji wa filamu anayependwa huku Hemmed PHD ameibuka mshindi wa wa tuzo ya muigizaji wakiume anayependwa na filamu ya Kigodoro imeibuka kuwa ni filamu inayopendwa.
Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania
Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati Mapinduzi hayo yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada ya tangazo la kupindulikwa kwake, Rais huyo alipanda ndege kurejea nchini kwake licha ya tangazo la kufungwa kwa mipaka yote na viwanja vya...
Comments
Post a Comment