Skip to main content

Yanga kuibeba Azam leo?

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Yanga, leo wanashuka dimbani kutafuta ushindi wa kunogesha sherehe za kupokea kombe lao katika mchezo dhidi ya Azam utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga wanatarajiwa kukabidhiwa kombe la ubingwa na mgeni rasmi katika mechi hiyo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara baada tu ya kumalizika kwa mechi hiyo itakayoanza saa 11 jioni.

Tayari kikosi hicho cha Jangwani kina pointi 55, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwa sasa ambazo walizifikisha katika mchezo wao uliopita dhidi ya Polisi Morogoro baada ya kuwafunga mabao 4-1.

Timu wanayokutana nao, Azam FC yenye pointi 45 ndio yenye presha kubwa kwani wanahitaji ushindi katika mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kubaki katika nafasi ya pili.

Iwapo Azam itapoteza mchezo huo na ujao dhidi ya Mgambo Shooting ya Tanga itakuwa kwenye mazingira magumu ya kumaliza katika nafasi ya pili, lakini ikitoka sare au kushinda mchezo ujao, basi itakuwa imeinyima Simba nafasi hiyo ambayo wanaisaka kwa udi na uvumba ili kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.

Kocha wa Azam FC, GeorgeNsimbe alisema anatarajia kikosi chake kitaondoka na ushindi katika mchezo huo. Nsimbe alisema ana imani kubwa na kikosi chake kinaweza kubadilisha matokeo na kuwa mazuri na hivyo kushika nafasi ya pili ili kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.

Wakati Azam FC wakijitamba kushinda, Yanga ambao waliwasili juzi wakitokea Tunisia wamesema wamejipanga kuondoka na ushindi katika mchezo huo ili kusherehekea vizuri kombe lao.

Pia, imewakata kauli baadhi ya watu wanaotoa vitisho dhidi yao kuwataka iwafunge Azam FC, kuwa isiwapangie na kwamba iiwaache wafanye wanavyofahamu wao.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema jana kuwa kumekuwa na minong’ono na taarifa kwenye mitandao kuwa kuna dalili za kupanga matokeo, jambo alilosema halipo na wala hawatarajii kuwepo.

“Tusipewe vitisho vya kumfunga Azam FC, hatuko kumbeba mtu… mbona wakati tukihangaika kwa jasho letu hamkuwepo, hata hao mashabiki wa Simba ambao wanatafuta undugu, mbona kwenye mechi yetu dhidi ya Etoile du Sahel waliishangilia Tunisia, watuache wenyewe,” alisema Muro.

Alisema kitendo cha Yanga kuchukua ubingwa mapema isiwe ni tatizo kwani hawako kutumika kwa wengine. Alisema kocha aachwe mwenyewe atajua ni kikosi gani ambacho atakipanga na kwamba asipangiwe wala kuingiliwa na watu na wakati huo huo, akiomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia wakikabidhiwa kombe lao.

Mechi hiyo itachezeshwa na Jacob Adongo (Mara), akisaidiwa na Frednand Chacha (Mwanza), Hellen Mduma (Dar es Salaam), mwamuzi wa akiba Hussein Kalindo (Dar es Salaam) na Kamishna ni Damian Mabena (Tanga).

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), sherehe za makabidhiano ya tuzo zitaenda sambamba na wadhamini wa ligi, Kampuni ya simu za mkononi Vodacom kumkabidhi zawadi mchezaji bora wa Aprili, mshabuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa atakayezawadiwa Sh milioni moja

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...