Skip to main content

Bunge kukaa hadi Jumapili

MKUTANO wa 20 wa Bunge la Bajeti kwa mwaka wa fedha 2015/16, umelazimika kupanga kikao chake kufanyika keshokutwa Jumapili ili kwenda na ratiba.

Kwa mujibu wa ratiba mpya ya Mkutano huo iliyotolewa jana na Ofisi ya Bunge, keshokutwa Wizara ya Fedha itawasilisha bajeti yake kuanzia saa tano asubuhi.

Awali, Wizara ya Fedha ilipangwa kuwasilisha bajeti yake kesho, lakini ratiba ilivurugika Jumanne wiki hii baada ya kifo cha ghafla cha Mbunge wa Jimbo la Ukonga mkoani Dar es Salaam, Eugen Mwaiposa (CCM).

Kutokana na kifo hicho, Bunge liliahirishwa Jumanne mchana ikiwa ni saa chache baada ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Bunge lilirejea jana kwa kipindi cha Maswali ya Kawaida asubuhi bila kuwapo kwa Maswali ya Papo kwa Hapo kwa Waziri Mkuu na baadaye mjadala wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii uliendelea hadi jioni.

Leo itakuwa zamu ya Wizara ya Maji na kesho itakuwa Wizara ya Nishati na Madini, wizara mbili ambazo hotuba zao zilitakiwa kuwasilishwa Jumatano na Ijumaa.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambayo hotuba yake ilipangwa kuwasilishwa jana, sasa itawasilishwa Jumatatu wiki ijayo.

Aidha, ratiba hiyo inaonesha kuwa na siku tatu za Serikali na Kamati ya Bajeti kufanya majumuisho kuzingatia hoja zenye maslahi kwa Taifa zilizojitokeza wakati wa kujadili Bajeti za Wizara, sasa zimepunguzwa na kuwa siku mbili, Jumanne na Jumatano ijayo.

Bajeti ya Serikali itasomwa kama ilivyopangwa Alhamisi ijayo ikitanguliwa asubuhi na Taarifa ya Hali ya Uchumi itakayosomwa na Waziri mwenye dhamana ya Mipango.

Comments

Popular posts from this blog

Mnyukano urais chama cha walimu

a Gratian Mukoba. MCHUANO mkali umeibuka ndani ya Chama cha Walimu Nchini (CWT) baada ya wagombea 28 kujitosa kuwania Urais wa chama hicho chenye nguvu kutokana na kuundwa na idadi kubwa ya watumishi wa umma. Miongoni mwa wanaogombea ni rais wa sasa wa chama hicho, Gratian Mukoba ambaye pia Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA). Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Alhamisi wiki hii kwenye Ukumbi wa hoteli ya Ngurdoto, Arumeru mkoani Arusha siku ambayo itakuwa inahitimisha mkutano mkuu wa siku tatu wa chama hicho unaotarajiwa kufunguliwa kesho na Rais Jakata Kikwete. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, Kanda ya Ziwa imeongoza kwa kutoa wagombea wengi wakiwemo wa mkoa wa Mwanza, Kaliyaya Masunga wa Ilemela, Magesa Kirati wa Kwimba, Marwa D. Marwa wa Nyamagana na Mashauri Benedict kutoka Sengerema. Wengine wa Kanda ya Ziwa ni Charles George wa Geita, Godi Kiduma, Lyangombe Dotto na Malimi Macheyeki kutoka Maswa mkoani Simiyu na Juma Boniface wa Bund...

Aunty Ezekiel ajifungua mtoto wa kike, amuita Cookie

Muigizaji wa filamu za Bongo, Aunty Ezekiel amejifungua mtoto wa kike siku ya Alhamis May 21. Mtoto huyo wa Aunty Ezekiel ambaye baba yake ni dancer wa Diamond aitwaye Mose Iyobo, amepewa jina la Cookie. Aunty ameshare habari hiyo na mashabiki wake wa Instagram: “Amin ktk Mungu ndio Mwisho wa Matatizo yote yaliyotuzunguka Hakuna mganga wala Mchawi pasipo Mungu. "Ahsante Mungu wang kwa kunikabidhi zawadi yang Asubuhi jana tar 21-05-2015 Muache yy atende kwani ndio nguzo yetu sote Nasema Ahsante tena Ahsante kwa zawadi hii kubwa ktk Maisha kwani ilikuwa ni kipindi kigumu chenye majaribu ya kila aina kupitia binaadamu wajizaniao wao ni miungu watu Bac endelea kunyoosha mkono wako ktk paji la kiumbe wako ukiwa kama kinga nami niwe kivuli tuu juu yake Amen Whn Jesus Say Yes Ni body can Say wht!!!!!!!Wlcm Baby Cookie wlcm 2 da world KIBOKO YANG…” Diamond ambaye ni uncle wa Cookie pia amempongeza Aunty na Mose kupitia Instagram: “Hongera sana @auntyezekiel na @...

Tanzanian Irene Kiwia Wins Woman of The Year Africa Award.

Africa Reconnect (http://www.africareconnect.com), a platform for women who have made remarkable contributions to the growth and development of the various nations in Africa has today awarded 11 Africans whose contributions to women empowerment in their countries is outstanding. The award ceremony, which took place in Polokwane, Limpopo South Africa, concluded a two day empowerment conference themed “ Accelerating Positive Change”. The 2015 awards recipient included; Seja Lorraine Semenya for best Cultural Developer in Africa, Dr. K. S Malukele for Best Community Developer in Africa, Mphatheleni Makaulele for Most Inspiring Woman in Africa, all from South Africa. The first lady of Akwibo State for Best Philanthropic in Africa and Irene Kiwia from Tanzania won Woman of the Year Africa award.