Mbunge wa Monduli ambaye aliwahi kuwa Waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa amaeahirisha kuchukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi hadi siku ya kesho ambayo ni alhamisi.
Hadi sasa mwanasiasa aliyefungua dimba la kuchukua fomu ya urais ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya pamoja na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira.
Mwanasiasa anayefuata mchana huu ni Amina Salum Ali.
a Gratian Mukoba. MCHUANO mkali umeibuka ndani ya Chama cha Walimu Nchini (CWT) baada ya wagombea 28 kujitosa kuwania Urais wa chama hicho chenye nguvu kutokana na kuundwa na idadi kubwa ya watumishi wa umma. Miongoni mwa wanaogombea ni rais wa sasa wa chama hicho, Gratian Mukoba ambaye pia Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA). Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Alhamisi wiki hii kwenye Ukumbi wa hoteli ya Ngurdoto, Arumeru mkoani Arusha siku ambayo itakuwa inahitimisha mkutano mkuu wa siku tatu wa chama hicho unaotarajiwa kufunguliwa kesho na Rais Jakata Kikwete. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, Kanda ya Ziwa imeongoza kwa kutoa wagombea wengi wakiwemo wa mkoa wa Mwanza, Kaliyaya Masunga wa Ilemela, Magesa Kirati wa Kwimba, Marwa D. Marwa wa Nyamagana na Mashauri Benedict kutoka Sengerema. Wengine wa Kanda ya Ziwa ni Charles George wa Geita, Godi Kiduma, Lyangombe Dotto na Malimi Macheyeki kutoka Maswa mkoani Simiyu na Juma Boniface wa Bund...
Comments
Post a Comment