Skip to main content

mashabiki Alikiba asema vurugu zilizotokea Afrika Kusini zimesababisha video ya ‘Chekecha’ ichelewe, awaomba msamaha mashabiki

Staa wa muziki Alikiba amesema kuwa video shooting ya wimbo wake ‘Chekecha’ ambayo imepangwa kufanyika Afrika Kusini, imechelewa kutokana na vurugu dhidi ya raia wa kigeni (Xenophobia) zilizoibuka hivi karibuni nchini humo.

“Tayari tulikuwa tumeplan kila kitu unajua kunakuwa kuna zile dancing, choreographer wangu alikuwa ameshacreate kila kitu amewatumia dancers wa South Africa, lakini kilichotufelisha ni hii Xenophobia iliyokuwa imetokea,” alisema Alikiba kupitia Ubaoni ya E-Fm. “Vile vile unajua vifaa kule wanakuwa wanaazima kwahiyo imekuwa ni sheria ambayo imepitishwa hairuhusiwi kufanya hivyo mpaka patulie.”

Hata hivyo Alikiba amesema mipango yote inaenda vizuri na siku si nyingi atasafiri kuelekea Afrika Kusini kwaajili ya kulipa deni la video alilonalo kwa mashabiki wake.

“Kwahiyo tumefanya tena opportunity nyingine tumepata tayari namshukuru Mungu tumeshapanga kila kitu.”

Kwa kuonesha kuwa anawajali na kuwaheshimu mashabiki, King Kiba hakusita kuwaomba msamaha kwa kuchelewa kufanya video ya ‘Chekecha’, wimbo ambao una karibia kufikisha miezi mitatu toka ulipoachiwa mwishoni mwa February.

“Mimi nataka kuchukua nafasi hii kukuomba samahani, mafans wangu wote na wapenzi wa muziki, najitahidi sana lakini sisi tunapanga yetu na Mungu anapanga yake

Comments

Popular posts from this blog

Mnyukano urais chama cha walimu

a Gratian Mukoba. MCHUANO mkali umeibuka ndani ya Chama cha Walimu Nchini (CWT) baada ya wagombea 28 kujitosa kuwania Urais wa chama hicho chenye nguvu kutokana na kuundwa na idadi kubwa ya watumishi wa umma. Miongoni mwa wanaogombea ni rais wa sasa wa chama hicho, Gratian Mukoba ambaye pia Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA). Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Alhamisi wiki hii kwenye Ukumbi wa hoteli ya Ngurdoto, Arumeru mkoani Arusha siku ambayo itakuwa inahitimisha mkutano mkuu wa siku tatu wa chama hicho unaotarajiwa kufunguliwa kesho na Rais Jakata Kikwete. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, Kanda ya Ziwa imeongoza kwa kutoa wagombea wengi wakiwemo wa mkoa wa Mwanza, Kaliyaya Masunga wa Ilemela, Magesa Kirati wa Kwimba, Marwa D. Marwa wa Nyamagana na Mashauri Benedict kutoka Sengerema. Wengine wa Kanda ya Ziwa ni Charles George wa Geita, Godi Kiduma, Lyangombe Dotto na Malimi Macheyeki kutoka Maswa mkoani Simiyu na Juma Boniface wa Bund...

Aunty Ezekiel ajifungua mtoto wa kike, amuita Cookie

Muigizaji wa filamu za Bongo, Aunty Ezekiel amejifungua mtoto wa kike siku ya Alhamis May 21. Mtoto huyo wa Aunty Ezekiel ambaye baba yake ni dancer wa Diamond aitwaye Mose Iyobo, amepewa jina la Cookie. Aunty ameshare habari hiyo na mashabiki wake wa Instagram: “Amin ktk Mungu ndio Mwisho wa Matatizo yote yaliyotuzunguka Hakuna mganga wala Mchawi pasipo Mungu. "Ahsante Mungu wang kwa kunikabidhi zawadi yang Asubuhi jana tar 21-05-2015 Muache yy atende kwani ndio nguzo yetu sote Nasema Ahsante tena Ahsante kwa zawadi hii kubwa ktk Maisha kwani ilikuwa ni kipindi kigumu chenye majaribu ya kila aina kupitia binaadamu wajizaniao wao ni miungu watu Bac endelea kunyoosha mkono wako ktk paji la kiumbe wako ukiwa kama kinga nami niwe kivuli tuu juu yake Amen Whn Jesus Say Yes Ni body can Say wht!!!!!!!Wlcm Baby Cookie wlcm 2 da world KIBOKO YANG…” Diamond ambaye ni uncle wa Cookie pia amempongeza Aunty na Mose kupitia Instagram: “Hongera sana @auntyezekiel na @...

Tanzanian Irene Kiwia Wins Woman of The Year Africa Award.

Africa Reconnect (http://www.africareconnect.com), a platform for women who have made remarkable contributions to the growth and development of the various nations in Africa has today awarded 11 Africans whose contributions to women empowerment in their countries is outstanding. The award ceremony, which took place in Polokwane, Limpopo South Africa, concluded a two day empowerment conference themed “ Accelerating Positive Change”. The 2015 awards recipient included; Seja Lorraine Semenya for best Cultural Developer in Africa, Dr. K. S Malukele for Best Community Developer in Africa, Mphatheleni Makaulele for Most Inspiring Woman in Africa, all from South Africa. The first lady of Akwibo State for Best Philanthropic in Africa and Irene Kiwia from Tanzania won Woman of the Year Africa award.