Skip to main content

Midahalo Watangaza Nia CCM Ruksa......Kinana Asema Nafasi Wanayoomba ni Kubwa, Ataka Wahojiwe wananchi Wawasikie

SIKU moja baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mohamed Seif Khatib kupiga marufuku pamoja na mambo mengine makada wa chama hicho waliochukua fomu kuwania urais kushiriki midahalo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana amepinga msimamo huo.

Badala yake, Kinana ameruhusu makada hao wanaoomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho kwa nafasi ya urais kushiriki katika midahalo iliyoandaliwa na Umoja wa Watendaji wa Kampuni binafsi (Ceo's roundtable), huku akiwataka waandaaji wa midahalo hiyo kutenda haki ili kuepusha mifarakano.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba jana, Kinana alisema midahalo hiyo inaweza kuwafanya wananchi kuwatambua wagombea wao na kuwapima kwa hoja kama wanaweza kuongoza nchi au la ili waweze kuwapigia kura.

“Nimepigiwa simu na baadhi ya wagombea waliotangaza nia ya kuwania nafasi ya urais ndani ya chama, sasa nawaambia kuwa wana hiari ya kwenda au kutokwenda kwa sababu ni uamuzi wao binafsi na si suala la chama.

“Wakati walipotangaza nia na kuchukua fomu walisema mengi sana ikiwamo jinsi watakavyoweza kuongoza nchi na wananchi wamewasikia, hivyo basi chama hakina uwezo wa kuwakataza kushiriki kwenye midahalo hiyo,” alisema.

Juzi Seif Khatib alikaririwa na vyombo vya habari akisema hakuna mgombea urais yeyote atakayeruhusiwa kushiriki midahalo hiyo hadi hapo chama kitakapompata mgombea mmoja wa nafasi hiyo.

Hata hivyo Kinana jana aliwaambia waandishi kuwa mdahalo huo si wa CCM, bali umeandaliwa na watendaji wengine ili kuwapima wagombea hao katika kipindi hiki wanachotaka kuwania nafasi ya uongozi.

Alisema haoni haja ya chama kuwakataza kushiriki katika midahalo hiyo wakati nafasi wanazozitaka ni za kitaifa na kimataifa ambazo zinawahusisha wananchi wenyewe, hivyo wanapaswa kushiriki ili waweze kupimwa.

“Chama hakiwezi kuwazuia watangaza nia kushiriki kwenye midahalo kwa sababu nafasi wanazoomba ni za kuwatumikia wananchi, kama kuna mdahalo ambao utawafanya kujibu hoja na kutoa ufafanuzi, wanachama wa CCM watawapima hoja zao na wananchi watawapima zaidi ili waweze kujua nani anayewafaa,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, walioandaa midahalo hiyo wanapaswa kutenda haki na si kuwabeba watangaza nia, jambo ambalo linaweza kuleta mifarakano isiyo na sababu.

“Lengo la midahalo iwe ni kuwasaidia wananchi kuwafahamu wagombea wao ili waweze kufanya uamuzi sahihi,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo waandaaji wanapaswa kuangalia masilahi ya wananchi  ili waweze kujua sera zao na kujenga hoja ambazo zitawasaidia kuwapima.

Kinana alisema midahalo hiyo isijenge chuki na kuleta mifarakano ambayo itawafanya wagombea kugombana, jambo ambalo linaweza kusababisha mifarakano

Comments

Popular posts from this blog

Mnyukano urais chama cha walimu

a Gratian Mukoba. MCHUANO mkali umeibuka ndani ya Chama cha Walimu Nchini (CWT) baada ya wagombea 28 kujitosa kuwania Urais wa chama hicho chenye nguvu kutokana na kuundwa na idadi kubwa ya watumishi wa umma. Miongoni mwa wanaogombea ni rais wa sasa wa chama hicho, Gratian Mukoba ambaye pia Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA). Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Alhamisi wiki hii kwenye Ukumbi wa hoteli ya Ngurdoto, Arumeru mkoani Arusha siku ambayo itakuwa inahitimisha mkutano mkuu wa siku tatu wa chama hicho unaotarajiwa kufunguliwa kesho na Rais Jakata Kikwete. Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, Kanda ya Ziwa imeongoza kwa kutoa wagombea wengi wakiwemo wa mkoa wa Mwanza, Kaliyaya Masunga wa Ilemela, Magesa Kirati wa Kwimba, Marwa D. Marwa wa Nyamagana na Mashauri Benedict kutoka Sengerema. Wengine wa Kanda ya Ziwa ni Charles George wa Geita, Godi Kiduma, Lyangombe Dotto na Malimi Macheyeki kutoka Maswa mkoani Simiyu na Juma Boniface wa Bund...

Aunty Ezekiel ajifungua mtoto wa kike, amuita Cookie

Muigizaji wa filamu za Bongo, Aunty Ezekiel amejifungua mtoto wa kike siku ya Alhamis May 21. Mtoto huyo wa Aunty Ezekiel ambaye baba yake ni dancer wa Diamond aitwaye Mose Iyobo, amepewa jina la Cookie. Aunty ameshare habari hiyo na mashabiki wake wa Instagram: “Amin ktk Mungu ndio Mwisho wa Matatizo yote yaliyotuzunguka Hakuna mganga wala Mchawi pasipo Mungu. "Ahsante Mungu wang kwa kunikabidhi zawadi yang Asubuhi jana tar 21-05-2015 Muache yy atende kwani ndio nguzo yetu sote Nasema Ahsante tena Ahsante kwa zawadi hii kubwa ktk Maisha kwani ilikuwa ni kipindi kigumu chenye majaribu ya kila aina kupitia binaadamu wajizaniao wao ni miungu watu Bac endelea kunyoosha mkono wako ktk paji la kiumbe wako ukiwa kama kinga nami niwe kivuli tuu juu yake Amen Whn Jesus Say Yes Ni body can Say wht!!!!!!!Wlcm Baby Cookie wlcm 2 da world KIBOKO YANG…” Diamond ambaye ni uncle wa Cookie pia amempongeza Aunty na Mose kupitia Instagram: “Hongera sana @auntyezekiel na @...

Tanzanian Irene Kiwia Wins Woman of The Year Africa Award.

Africa Reconnect (http://www.africareconnect.com), a platform for women who have made remarkable contributions to the growth and development of the various nations in Africa has today awarded 11 Africans whose contributions to women empowerment in their countries is outstanding. The award ceremony, which took place in Polokwane, Limpopo South Africa, concluded a two day empowerment conference themed “ Accelerating Positive Change”. The 2015 awards recipient included; Seja Lorraine Semenya for best Cultural Developer in Africa, Dr. K. S Malukele for Best Community Developer in Africa, Mphatheleni Makaulele for Most Inspiring Woman in Africa, all from South Africa. The first lady of Akwibo State for Best Philanthropic in Africa and Irene Kiwia from Tanzania won Woman of the Year Africa award.