Skip to main content

Padre na Wanafunzi sita Wateteketea Kwa Moto

WANAFUNZI sita wa Sekondari ya CTC Kigonsera inayomilikiwa na Misheni ya Mbinga mkoani Ruvuma na Mkuu wa Shule hiyo, Padre Yazint Kawonga, wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia bondeni kisha kuwaka moto na kuiteketeza miili yao.

Akizungumza na Mpekuzi jana shuhuda wa ajali hiyo, Makarius Nchimbi, alisema ilitokea juzi saa tisa alasiri katika mlima uliopo karibu na shule hiyo huku likiwa limewabeba wanafunzi waliokuwa wakitokea shambani kuvuna mahindi ya shule hiyo.

Nchimbi ambaye ni mfanyakazi wa kitengo cha udereva katika misheni hiyo alidai yeye ndiye aliyekuwa dereva wa gari hilo kabla ya kupokelewa na Padre Kawonga aliyemtaka amsaidie kuliendesha kwa kuwarudisha shuleni wanafunzi waliokuwa shamba lililopo Kijiji cha Mkulumus kilichopo Kigonsera.

Alisema gari hilo aina ya Land Rover 110 Station Wagon lenye namba T 306 AYM  lilipofika katika mlima huo lilimshinda Padre Kawonga wakati akitumia gia namba mbili na kuanza kurudi nyuma huku wanafunzi wengine waliokaa juu walifanikiwa kuruka kabla halijatumbukia na baadhi yao 24 waliumia.

Alisema baada ya gari hilo kutumbukia bondeni wao walijitahidi kuingia kwenda kuvunja milango ili waweze kuwaokoa baadhi yao lakini ilishindikana kutokana na nyaya za umeme wa gari kulipuka na kuliunguza huku miili yao ikiwemo ndani  na kusababisha ishindwe kutambulika.

Alisema kutokana na moto kuwaka iliwalazimu watafute mbinu za kuuzima na walitumia maji lakini haikuwezekana na walifanya jitihada ya kuipata winchi iliyoweza kwenda kuliinua gari hilo likiwa limeteketea.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kigonsera, Dk. Patrik Mhagama, alisema kituo hicho kilipokea maiti saba na majeruhi wakiwa 24 na kati ya hao wawili wamepekwa Hospitali ya Mbinga kutokana na hali zao kuwa mbaya huku 17 walitibiwa na kuruhusiwa na watano bado wapo kituoni hapo.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikihela, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na alisema taratibu za kuyapata majina halisi ya marehemu bado zinaendelea na zikikamilika zitatolewa taarifa.

Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Japheth Komba (16), Regobert Mahai (16), Edgar Maseko (16), Luiza Mbunda, Afa Kifaru (15), Nelalfred Nchimbi (16), Teodora Wolfa (16).

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...