Skip to main content

Polisi yakamata kontena la nyaya za milioni 150/-

Maalumu ya Dar es Salaam limekamata kontena likiwa na rola 15 za nyaya za umeme mali ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zenye thamani ya Sh milioni 150.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro, alisema nyanya hizo ziliibwa Februari 26 zikiwa zinasafirishwa kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Alisema baada ya wizi wa kontena hilo, kesi ilifunguliwa katika Kituo cha Polisi Buguruni na watuhumiwa watano kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Aliongeza kuwa wakati upelelezi ukiendelea Mei 25 mwaka huu, polisi walipokea taarifa kutoka kwa msiri kwamba maeneo ya Kibamba mtaa wa Kibengewe kuna kontena katika kiwanda cha kutengenezea matofali.

Alisema askari walifika eneo la tukio na kukuta kontena hilo lenye namba 00LU2876031 na kumhoji mlinzi wa eneo hilo ili kumpata mmiliki wa eneo na kontena hilo.

“Tunashukuru ilipofika saa 5:00 usiku tulifanikiwa kumpata mmiliki wa eneo hilo, Donesia Aidan (40) ambaye ni mfanyabiashara mkazi wa Mbezi makabe,” alisema Sirro.

Alisema taratibu zilikamilika na askari walifungua kontena hilo na zilikutwa rola za nyaya zipatazo 15 kati ya 17 zilizokuwepo katika kontena hilo siku lilipokuwa likisafirishwa.

Pia alisema jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata mtu mwingine anayehusika katika wizi wa kontena hilo, Prosper Mtei (43) ambaye ni mfanyabiashara na upelelezi unaendelea ili aweze kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi ya

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Frola Mbasha Ajiunga CHADEMA

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio. ” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee. Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti. Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata...