Skip to main content

WEMA SEPETU Awashukia na Kuwapa Vidonge vyao Waandaji wa Instagram Kwa Kutokumlipa Mzee Majuto

Wema Sepetu Amefunguka kwenye Ukurasa wake wa Instagram akiwachana waandaji wa Instagram Parties Kwa Kutokumlipa Mzee Majuto Pesa zake baaada ya Wema Kuwaunganishia Mzee Huyo ili Aje kwenye Party yao iliyofanyika week end iliyopita Hapa Dar es Salaaam.....Ameandika Hivi:

    Waandaaji wa Instagram party sijawapenda kiukweli... Mpaka nimefkia hatua ya kuandika basi mjue kuwa mmenikwaza... Mlikuja kwangu na mkaniomba niwatafutie Huyu Mzee wa watu... Kwa moyo mmoja nilifanya hivyo, Iweje leo hii kashamaliza kazi msitake kumlipa hela yake... Baba wa watu katoka Tanga na nauli yake, mpaka hotel kajilipia mwenyewe.... Mimi sipendi lawama jamani... Sana sana ikiwa ni kwa wasanii wenzangu... Sasa hivi naonekana mbaya mimi maana mimi ndo niliewaunganisha na huyu Baba wa watu... Hawawajui nyie ananijua mimi..... Na kaja kwa heshima yangu.... Hizo ni dhulma na sio vizuri kumfanyia hivyo Mzee wa watu... Namuheshimu sana na siwezi kumkosea heshima kiasi hicho... Ila hakuna neno tumwachie Mungu sio..... @instagrampartytz @instagrampartytz ... Kiukweli siwezi kuja kufanya kazi na watu kama nyie at all.... You are nat Loyal..... Plz repost it

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Aunty Ezekiel ajifungua mtoto wa kike, amuita Cookie

Muigizaji wa filamu za Bongo, Aunty Ezekiel amejifungua mtoto wa kike siku ya Alhamis May 21. Mtoto huyo wa Aunty Ezekiel ambaye baba yake ni dancer wa Diamond aitwaye Mose Iyobo, amepewa jina la Cookie. Aunty ameshare habari hiyo na mashabiki wake wa Instagram: “Amin ktk Mungu ndio Mwisho wa Matatizo yote yaliyotuzunguka Hakuna mganga wala Mchawi pasipo Mungu. "Ahsante Mungu wang kwa kunikabidhi zawadi yang Asubuhi jana tar 21-05-2015 Muache yy atende kwani ndio nguzo yetu sote Nasema Ahsante tena Ahsante kwa zawadi hii kubwa ktk Maisha kwani ilikuwa ni kipindi kigumu chenye majaribu ya kila aina kupitia binaadamu wajizaniao wao ni miungu watu Bac endelea kunyoosha mkono wako ktk paji la kiumbe wako ukiwa kama kinga nami niwe kivuli tuu juu yake Amen Whn Jesus Say Yes Ni body can Say wht!!!!!!!Wlcm Baby Cookie wlcm 2 da world KIBOKO YANG…” Diamond ambaye ni uncle wa Cookie pia amempongeza Aunty na Mose kupitia Instagram: “Hongera sana @auntyezekiel na @...