Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2018

Lukuvi afunga ofisi nzima, ageukia wamiliki viwanja

 Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, William Lukuvi jana alifunga ofisi za ardhi na masijala za Jiji la Dar es Salaam, akisema anafunga mtambo wa kufyatua migogoro ya ardhi. Waziri Lukuvi pia amewaonya wamiliki katika Mradi wa Viwanja 20,000 kukaa chonjo kwa kuwa wanaweza kunyang’anywa, huku akiagiza kuanza kwa msako wa watu waliotelekeza hati 6,000 za umiliki wa viwanja zilizotolewa na wizara yake takribani miaka 20 iliyopita. Lakini, moto ulikuwa ofisi ya ardhi ya Jiji la Dar es Salaam ambako Waziri Lukuvi alitaka maofisa hao wakusanye nyaraka za ofisi yao na kuhamia wizarani kwa kuwa hawana cha kufanya eneo hilo. “Mnajua kwa muda mrefu nimekuwa nikipambana na migogoro ya ardhi nchini, leo imefika tamati. Nimeshagundua chanzo chake kinatokea hapa. Nazifunga hizi ofisi,” alisema Waziri Lukuvi. “Hizi ofisi zinatoa hati zisizotambulika kwa kisingizio cha ofa. Mtu yeyote mwenye ofa ya kiwanja na ina muhuri wa jiji haitambulik...