Skip to main content

Posts

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...

Hotuba ya Mh. Steven Wassira Aliyoitoa Leo Jijini Mwanza Wakati Akitangaza Nia ya Kugombea Urais wa Tanzania Kupitia CCM

Nianze kwa kutoa shukrani kwenu wote mlioacha shughuli zenu ili kuja hapa kunisikiliza. Kuja kwenu hapa kwa wingi ni ishara ya imani mliyonayo kwangu, Nawashukuru sana     Kwa zaidi ya mwaka mzima, kumekuwepo na miningo’no kuhusu uwezekano wangu kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Aidha kutokana na mijadala ya wananchi au kupitia mitandao ya kijamii au vyombo rasmi vya habari, mining’ono hiyo imefanya baadhi ya watu wanifuate ili wanishauri nigombee na wengine wamenipigia simu kwa kunishawishi nisisite kugombea     Leo, nakuja hapa Mwanza kuvunja ukimya na kumaliza minong’ono kwa kutangaza rasmi kwamba nimekata shauri kugombea nafasi ya urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania KWANINI NAGOMBEA Zikosababu kadhaa, ambazo zimenisukuma kugombea kufikia uamuzi huo     Haki yangu ya kikatiba. Hii ni sababu ya msingi lakini siyo yenye uzito, kwa vile ni haki ya kikatiba na ni kwa ajili ya watanzania wote. Hivyo...

Nancy Sumary na Dada Yako Nakaya Kunani ? Je ni Kweli Kuna Beef Kati ya Hawa Ndugu Wawili?

Nasikia Habari ya Mjini ni kuwa Hawa Ndugu wawili wa Damu Nancy Sumary na Dada yake Nakaya Kwa sasa Haziivi Hata Kidogo...Je Kunani Ama ni Uzushi tu ...Embu kwa Anaye jua A-Z atujuze....Maana Sitaki Kuamini Jinsi walivyokuwa wanapendana..eti sasa kila mtu kivyake.... Udaku Special Blog

Baada ya Jana Lowassa Kutangaza nia Urais 2015..January Makamba Nae Aja na Mpya

Tume ya taifa ya uchaguzi imeshatangaza kwamba uchaguzi mkuu utafanyika October 2015 ambapo sasa ni headlines zake zinachukua nafasi kwa watu mbalimbali kutangaza nia za kugombea nafasi ya juu ya Urais. Post hii inamilikiwa na January Makamba ambae ni Mbunge wa Bumbuli Tanga na anautaka Urais pia ambapo May 30 2015 aliandika :      ‘Wiki ijayo tutataarifu ni lini na kwa namna gani tutazungumza na Watanzania, kuchukua fomu, kuanza safari za mikoani kukutana na Watanzania‘ Udaku

Mrembo Jokate Amlipua Diamond, Ni Baada ya Kuitwa 'Makombo'

Jino kwa jino! Sexy lady anayefanya poa na ngoma yake ya Leo Leo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, amemlipua aliyewahi kuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye hivi karibuni alimwita makombo baada ya kusikia kwa sasa anatoka kimalovee na msanii Ali Kiba. Akizungumza na gazeti namba moja la mastaa Bongo, Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Jokate alisema alishangazwa na maneno hayo ambayo hakustahili kuyatamka kwani kama ni ishu ya mtu kula makombo mbona hata yeye ni makombo na bado anakula makombo? “Sijapendezwa na kauli ya Diamond na namshangaa sana, sijajua nini kimemkuta maana mimi sijamtaka wala hakuna ambapo niliwahi kumwambia kuwa ninatoka  au ninamtaka Kiba, zaidi ya maneno ya watu kwenye mitandao ya kijamii. “Hata kama hilo lipo, bado sioni maana ya neno makombo kwani hata yeye ni makombo na anakula makombo kwa Zari (Zarinah Hassan) kwani nani asiyejua?” alihoji Jokate akionekana kuchukizwa na kauli hiyo ya Diamond na ...

Diamond awapa somo wenzake

NYOTA wa muziki wa bongo flava nchini, Diamond Platinumz amewataka wasanii wa Tanzania kusambaza nyimbo zao kwa njia ya teknolojia ili kunufaika na jasho lao. Diamond aliyasema hayo wakati akizindua teknolojia ya muziki ili kuziingiza sokoni kazi zake baada ya kushauriana na wadau anaoshirikiana nao kikazi ambayo pia yeye ni balozi anayeitangaza. Amesema sababu kubwa iliyomsukuma kufanya biashara ya muziki kupitia progamu hii ni kwamba nyimbo zake ziweze kuwafikia mashabiki wake popote na muda wowote kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi na anakuwa na uhakika wa kupata mapato tofauti na zinavyosambazwa na wasambazaji wa mtaani. “Duniani kuna ushindani katika nyanja zote, hivyo sisi wanamuziki wa Tanzania tunapaswa kuhakikisha tunatoa muziki wa viwango vya juu kuhakikisha tunalenga zaidi katika masoko ya ndani na nje kama wenzetu wanavyofanya kusambaza kazi zao kupitia kampuni zinazotumia teknolojia ya kisasa na kumnufaisha msanii. “Kuna umuhimu mkubwa wa kujiamini, kuf...

Afungwa miaka 30 kwa kumbaka mtoto wa miaka tisa

Mkazi wa Malampaka mkoani Simiyu, Benedictor Bulobo (30) , ametupwa gerezani atakakotumikia kifungo kwa miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti wa miaka tisa. Alihukumiwa  na Mahakama ya Wilaya ya Maswa juzi na Hakimu Mwandamizi Mfawidhi  Agatha Chigulu, baada ya kuridhishwa  na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka. Akitoa hukumu hiyo hakimu huyo alisema kuwa anatoa adhabu hiyo ili kukomesha vitendo hivyo na kuwaonya wenye nia  mbaya ya kutaka kutenda kosa kama hilo wajifunze na kuacha mwenendo huo. Chigulu alieleza kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 131 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012. Awali mahakama iliambiwa na  Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Nassibu Swedy kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 23 mwaka jana  saa 5:00 asubuhi. Alimnajisi mtoto huyo  maeneo ya nyumbani kwake baada ya kumkamata  kwa nguvu binti huyo mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya M...