Skip to main content

Comoro yahitaji Msaada wa Ndege Tanzania

SERIKALI ya Comoro imeiomba Serikali ya Tanzania iisaidie kutatua changamoto ya uhaba wa ndege zinazotua nchini humo hali iliyosababishwa na kusitishwa kwa huduma za safari za shirika la ndege la Yemen.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi wa Comoro,  Bahia Masoundi, alisema Shirika la Ndege la Yemen lilisitisha huduma zake kufuatia machafuko yanayoendelea nchini Yemen.

“Mchafuko ya nchini Yemen yalipelekea shirika lao la ndege kusitisha huduma zake na kutokana na kwamba ndilo shirika tulilokuwa tukilitegemea kwa kiasi kikubwa ndio maana uhaba umejitokeza baada ya kufunga huduma zao,” alisema Massoundi.

Alisema kwa sasa kuna mashirika manne tu yanayofanya kazi nchini humo na ndege zinazotua ni chache na kwamba serikali ya nchi hiyo haimiliki shirika hata moja hivyo kulazimika kuomba msaada nchini Tanzania.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA), Charles Chacha alisema waziri huyo amefanya mazungumzo na waziri wa Uchukuzi nchini, Samweli Sitta ambaye ametoa maagizo kwa TCAA ili ifanye utaratibu wa kuisaidia nchi hiyo.

“Tayari tumepokea maagizo ya Waziri mwenye dhamana na sisi kama mamlaka inayosimamia safari za anga tunaanza mara moja kuangalia namna ya kuisaidia Comoro kwasababu ni nchi ambayo ina makubaliano ya kusaidiana na Tanzania,” alisema Chacha.

Alisema kwa sasa ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) hufanya safari zake mara nne kwa wiki nchini Comoro lakini bado kuna tatizo la mrundikano wa abiria wanaotaka kusafiri kwenda au kuja nchini kwa shughuli za biashara, utalii au kufuata huduma.

Aliongeza kutokana na uwezo mdogo wa ATCL atakutana na uongozi wa mashirika yenye uwezo yanayofanya kazi nchini yaweze kufanya safari nchini Comoro pamoja na kutoa kibali maalumu kwa shirika la ndege la Ethiopia ili ndege zake ziende nchini humo baada ya kutua Tanzania

Comments

Popular posts from this blog

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya...

Diamond Amuita Jokate Makombo...."Mwacheni Ali Kiba Ajilie Makombo"

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo. Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba. Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki. Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya. “Hamna jipya waache waendelee kumpigia...

Gharama za kupima ardhi kupunguzwa

SERIKALI imesema katika mwaka ujao wa fedha itapunguza gharama za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwawezesha wanachi kupima maeneo yao, hali ambayo inaonekana itapunguza migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa ziara mkoani hapa kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa miaka mingi. Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora, Waziri Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu, gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati ya umiliki. Lukuvi aliongeza kuwa serikali pia itaweza kukusanya kwa wingi kodi ya pango la ardhi, hivyo kuongeza mapato ambayo yataisaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Pamoja na kupunguza gharama hizo, Lukuvi aliwaonya maofisa ardhi kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu, akitolea mfano wa maofisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa lina...