0
Written by Hellen Mlacky
Hits: 6
WAPENZI wa soka nchini sasa watafaidi kwa kutazama michuano ya Kombe la Dunia chini ya miaka 20 mwaka 2015 moja kwa moja kwenye runinga zao kupitia ving’amuzi vya StarTimes.
Michuano hiyo ambayo itaanza kutimua vumbi Mei 30 na kumalizika Juni 20 mwaka huu, itaoneshwa moja kwa moja kutoka nchini New Zealand, ambapo timu 24 za vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani yatachuana kuwania ubingwa.
Akizungumza baada ya kupata haki miliki kutoka kwa FIFA za kutangaza michuano hiyo maarufu duniani ambayo hubeba mastaa wa baadae kwa timu zao za taifa, Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif alisema kuwa wana furaha kubwa kuonesha michuano hiyo kwani soka ni mchezo unaopendwa zaidi duniani.
Wapenzi wa soka wataweza kujionea mechi 52 kutoka timu 24 tofauti, ambapo mchezo wa kwanza utapigwa leo Mei 30 kwa kuwakutanisha wenyeji New Zealand na Ukraine.
Comments
Post a Comment