MSAFARA wa Makongoro Nyerere, mtoto wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, umepata ajali wakati mwanasiasa huyo akiwa katika harakati za kutimiza masharti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania nafasi ya urais.
Ajali hiyo iliyojeruhi watu watano waliokuwa kwenye msafara huo, ilitokea jana katika eneo la Tekniko, Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma baada ya gari aina ya Land Cruiser lenye namba T 188 BXG walilokuwamo kupinduka.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ferdinand Mtui, alisema ilitokea saa 10:30 asubuhi wakati msafara huo ukiongozwa na Makongoro ukielekea Kigoma mjini.
Kamishna Mtui aliwataja waliojeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwamo kichwani na mabegani kuwa ni dereva wa gari hilo Julius Kambarage, ambaye ni mtoto wa Makongoro na mwandishi Evans Magege.
Wengine ni Katibu Mwenezi wa CCM, Musoma Mjini, Fikiri Marumba na Ally Tesha ambao wote walipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu na kuendelea na msafara.
Majeruhi mwingine ni Cyprian Msiba ambaye ni mwandishi wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten ambaye alibaki hospitalini hapo kwa ajili ya huduma ya X-Ray kutokana na kuumia sehemu za bega.
Makongoro ambaye ni mbunge wa Afrika Mashariki, anazunguka mikoa mbalimbali nchini kwa nia ya kutafuta wadhamini ili kuomba ridhaa ya CCM kumpitisha kugombea nafasi ya urais.
Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania
Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani. Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Wakati Mapinduzi hayo yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu. Baada ya tangazo la kupindulikwa kwake, Rais huyo alipanda ndege kurejea nchini kwake licha ya tangazo la kufungwa kwa mipaka yote na viwanja vya...
Comments
Post a Comment