Hits: 215
Rais Jakaya KikweteRais Jakaya Kikwete
RAIS Jakaya Kikwete jana alianza ziara rasmi ya wiki moja katika nchi tatu za Ulaya kwa mwaliko wa viongozi wa nchi hizo.
Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini usiku wa kuamkia jana baada ya kumaliza kuendesha Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Burundi, ameanzia ziara yake katika Finland ambako atakaa kwa siku tatu.
Baadaye, Rais Kikwete atatembelea nchi za Sweden na Uholanzi kabla ya kurejea nyumbani.
Akiwa Finland, Rais Kikwete miongoni mwa mambo mengine leo atafanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali na Rais wa nchi hiyo na baadaye atatembelea Bunge.
Comments
Post a Comment