Skip to main content

Posts

CAR FROM JAPAN

http://click.carfromjapan.com/track/click/30577300/carfromjapan.com?p=eyJzIjoiTFQ2OF9jcldlNVZ4MGNmLWtnUHFYX2hwck8wIiwidiI6MSwicCI6IntcInVcIjozMDU3NzMwMCxcInZcIjoxLFwidXJsXCI6XCJodHRwczpcXFwvXFxcL2NhcmZyb21qYXBhbi5jb21cXFwvZW5cXFwvY2FtcGFpZ25cXFwvZ2l2ZWF3YXkteG1hcy0yMDE2P3JlZmVyPTU4NDFkMmMzMWExZjg5MDEwMDc4NDA3ZCZ1dG1fbWVkaXVtPWVtYWlsJnV0bV9zb3VyY2U9dHJhbnNhY3Rpb25hbCZ1dG1fY2FtcGFpZ249Y2FtcGFpZ24td2VsY29tZVwiLFwiaWRcIjpcIjAyMGE0ZjgwMTkxMjQ4N2I4NDc3NDUwNGYyOGRlMjA3XCIsXCJ1cmxfaWRzXCI6W1wiYmQ3ZGM4ZDg0ODc1NWU5MzAyMDY3Njc3ZjY2Njc5ZWQ2NjE2MzIwNVwiXX0ifQ

Membe kupeleka nchi kwenye uchumi wa viwanda

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ametangaza rasmi kuwania urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM}, huku akitamba ataipeleka nchi katika uchumi wa viwanda unaobebwa na kilimo na kuahidi kujenga serikali ya waadilifu. Licha ya Membe, wana CCM wengine wawili jana walitangaza pia kugombea urais nao ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Januari Makamba pamoja na Mbunge wa Nzega Dk Hamis Kigwangala. Membe alifichua kuwa alienda kuomba kwenye kaburi la Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere ili kupata ridhaa na kusisitiza kuwa urais si suala la kukurupuka na kwamba atahakikisha anasimamia utawala bora, huku akiongoza mapambano dhidi ya rushwa na kwa kubadili kipengele cha mtu atakayetoa rushwa na kutoa taarifa awe huru. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya CCM Mkoa wa Lindi jana, Waziri Membe alisema kabla ya kuchukua uamuzi wa kufikiria urais alijipima na kuona anatosha kwa nafasi hiyo, pia baada ya kuwaangali...

Mama amchoma mikono mwanae kwa madai ya kuiba ugali

i Mponzi mkazi wa kijiji cha Ikule wilayani Kilombero,  mkoani Morogoro anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma mwanae na kumjeruhi mikono kwa madai ya kuiba ugali. Mama huyo alimuunguza mwanaye  Joseph Chawala, akimtuhumu Kuiba Ugali, kwa mujibu wa watendaji  mbalimbali wa kata ya Mng’eta. Wakizungumzia tukio hilo Jerome Chulu na Jeneth Hetela,  walisema unyanyasaji huo  ulishuhudiwa na majirani wa mwanamke huyo baada ya kusikia kelele za watoto ambao walimchukua mtoto huyo kumpeleka ofisi  ya mtendaji wa kata,polisi na baadaye hospitali. Walibainisha baadaye kuwa polisi  walikwenda kumkamata mwanamke huyo na mumewe Halidi Kiwenji ambaye  inadaiwa alikuwa karibu wakati wa tukio hilo ingawa baadaye baba huyo aliachiwa ili akawaangalie watoto wengine nyumbani. Polisi  walithibitisha tukio hilo ambalo uchuguzi wake unaendelea ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo. Wananchi mbalimbali waliohojiwa wametaka hatua kuchukuliw...

Midahalo Watangaza Nia CCM Ruksa......Kinana Asema Nafasi Wanayoomba ni Kubwa, Ataka Wahojiwe wananchi Wawasikie

SIKU moja baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mohamed Seif Khatib kupiga marufuku pamoja na mambo mengine makada wa chama hicho waliochukua fomu kuwania urais kushiriki midahalo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana amepinga msimamo huo. Badala yake, Kinana ameruhusu makada hao wanaoomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho kwa nafasi ya urais kushiriki katika midahalo iliyoandaliwa na Umoja wa Watendaji wa Kampuni binafsi (Ceo's roundtable), huku akiwataka waandaaji wa midahalo hiyo kutenda haki ili kuepusha mifarakano. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba jana, Kinana alisema midahalo hiyo inaweza kuwafanya wananchi kuwatambua wagombea wao na kuwapima kwa hoja kama wanaweza kuongoza nchi au la ili waweze kuwapigia kura. “Nimepigiwa simu na baadhi ya wagombea waliotangaza nia ya kuwania nafasi ya urais ndani ya chama, sasa nawaambia kuwa wana hiari ya kwenda au kutokwenda kwa sababu ni uamuzi wao binafsi na si suala la chama. ...

Polisi yakamata kontena la nyaya za milioni 150/-

Maalumu ya Dar es Salaam limekamata kontena likiwa na rola 15 za nyaya za umeme mali ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zenye thamani ya Sh milioni 150. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro, alisema nyanya hizo ziliibwa Februari 26 zikiwa zinasafirishwa kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Alisema baada ya wizi wa kontena hilo, kesi ilifunguliwa katika Kituo cha Polisi Buguruni na watuhumiwa watano kukamatwa na kufikishwa mahakamani. Aliongeza kuwa wakati upelelezi ukiendelea Mei 25 mwaka huu, polisi walipokea taarifa kutoka kwa msiri kwamba maeneo ya Kibamba mtaa wa Kibengewe kuna kontena katika kiwanda cha kutengenezea matofali. Alisema askari walifika eneo la tukio na kukuta kontena hilo lenye namba 00LU2876031 na kumhoji mlinzi wa eneo hilo ili kumpata mmiliki wa eneo na kontena hilo. “Tunashukuru ilipofika saa 5:00 usiku tulifanikiwa kumpata mmiliki wa eneo hilo, ...

Wananchi wanaopata maji wafikia 55%

Jumanne Maghembe. SERIKALI imesema kwamba sekta ya maji kwa kutumia mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) imeongeza wananchi wanaopata huduma ya maji kutoka milioni 15.2 Juni, 2013 hadi kufikia milioni 20.9 sawa na asilimia 55. Hata hivyo, baadhi ya wabunge na Kambi Rasmi ya Upinzani wamepinga takwimu hizo. Aidha wabunge waliozungumza baada ya bajeti kusomwa jana, wabunge hao walisema kwamba kuna udanganyifu mkubwa wa takwimu zilizowasilishwa ndani ya Bunge, huku Kambi ya Upinzani ikidiriki kusema kwamba mipango ya Serikali ya kuwapatia wananchi wake maji imeshindwa. Msemaji wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Maji, Mohamed Rajab Mbarouk alisema kwamba takwimu za utafiti wa kitaifa katika eneo la maji, zinaonesha kwa sasa wananchi wanaopata maji safi na salama ni asilimia 40 tu na sio asilimia 57.8 kama ilivyorekodiwa katika taarifa za Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (Mkukuta). Alisema takwimu nyingi pamoja na visima vinavyofanya kazi si sahihi, hali inayodhihi...